Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

Kambi ya Watoto na Vijana Kutoka Shinyanga na Simiyu (Ariel Camp 2016) Yafungwa Mkoani Kilimanjaro


Kambi ya Ariel ya mwaka 2016 (Ariel Camp 2016) iliyodumu kwa muda wa siku tano kwa watoto na vijana 50 kutoka mikoa ya Shinyanga na Simiyu iliyoandaliwa na shirika la Ariel Glaser Pediatric AIDS Healthcare Initiative (AGPAHI) linalojihusisha na mapambano dhidi ya Virusi vya Ukimwi (VVU) na Ukimwi imefungwa.



Kambi hiyo ya 6 iliyokuwa na kauli mbiu isemayo "Watoto na Vijana ni hazina : Wape Kipaumbele katika huduma za afya na makuzi ili kuzuia maambukizi mapya ya VVU", ilianza siku ya Jumatatu,Juni 13,2016 na kumalizika siku ya Ijumaa, Juni 17,2016.

 Lengo la kambi ilikuwa kuwapatia watoto na vijana maarifa mbalimbali yatakayowawezesha kukua na kuishi katika matumaini chanya.

Akizungumza wakati wa kufunga kambi hiyo katika viwanja vya Hoteli ya Lutheran Uhuru mjini Moshi mkoani Kilimanjaro, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la AGPAHI, Dr. Sekela Mwakyusa ambaye pia ni rais wa Chama Cha Madaktari Bingwa wa Watoto Tanzania, alisema washiriki wa kambi hiyo ni watoto na vijana kutoka klabu 50 za watoto kutoka kwenye kliniki za huduma za dawa na matunzo katika mikoa hiyo.


“Lengo la klabu hizo ni kuwaleta pamoja watoto na vijana walio katika huduma ya tiba na matunzo ili kufahamu hali zao za kiafya, kufuatilia huduma za afya kwa urahisi, kupata ujasiri wa kuendelea na malengo yao na kutimiza ndoto zao”,aliongeza Dr. Mwakyusa.


Alibainisha kuwa klabu hizo pia zinasaidia watoto kuelimisha watoto wenzao, kusaidia watoto wenzao kufika katika huduma za afya kwa wakati lakini pia ni sehemu ya kucheza pamoja na kupeana matumaini mapya na njia mojawapo ya kuwahamasisha watoto na vijana kuendelea kubaki kwenye huduma.


“Tumejitahidi kwa kiasi kikubwa kuwafikia watoto na watu wazima wenye maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi (VVU) na kuwaanzishia huduma ya tiba na matunzo,hata hivyo kazi hii ni nzito,tunahitaji ushirikiano wa hali ya juu kutoka serikalini na wadau mbalimbali ili kuhakikisha kuwa tunapunguza hata kumaliza kabisa maambukizi ya VVU”,aliongeza Dr. Mwakyusa.


Awali akisoma historia ya klabu za watoto na kambi ya Ariel, Afisa miradi huduma unganishi kwa jamii AGPAHI, Richard Kambarangwe , alisema kambi zilianza baada ya klabu za watoto kuimarika, ndipo shirika la AGPAHI likaanzisha utaratibu wa kuwakutanisha watoto wanachama wa klabu katika kambi (Ariel children camp) ambapo watoto kutoka kila halmashauri za wilaya wakiwawakilisha wenzao kushiriki katika kambi.


Naye Afisa Mradi kitengo cha tiba na matunzo mpango wa taifa wa kudhibiti Ukimwi, Dr. Florence Ndaturu,mbali na kulipongeza shirika la AGPAHI kwa jitihada kubwa linazofanya katika mapambano dhidi ya VVU na Ukimwi hususani kwa mama na mtoto,aliyataka mashirika na taasisi zingine kuiga mfano kutoka AGPAHI.


“Asilimia kubwa ya watoto wanapata maambukizi ya VVU kutoka kwa mama,AGPAHI wanasaidia katika kutoa huduma ya kuzuia maambukizi ya VVU kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto,wanaisaidia serikali kwa kiasi kikubwa kuwaanzia tiba na kuwapa matunzo wale wote wanabainika kuwa na maambukizi na kuhakikisha kuwa hawapati maambukizi mapya ya VVU”, alisema Dr. Ndaturu.


Naye mwakilishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Paul Shayo alilishukuru shirika hilo kwa kujali afya ya watanzania na kuwaomba kuwafikia watanzania wengi zaidi katika mikoa mingine.


Nao watoto na vijana walioshiriki kambi hiyo,walieleza kufurahishwa na kambi hiyo kwani wameweza kucheza pamoja,kupata maarifa mbalimbali na kuongeza uelewa wa kijiografia baada ya kutembelea maeneo ya vivutio mkoani Kilimanjaro kama vile ziwa Chala.


Wakiwa kambini watoto na vijana hao walishiriki pia katika shindano la kutafuta mrembo wa kambi “Miss Ariel Camp 2016”,na mtanashati wa kambi “Mr. Ariel Camp 2016”,ambapo washindi walikuwa Winfrida Paul na Peter Kulwa.


Wakati wa kufunga kambi hiyo,watoto na vijana hao walipewa zawadi mbalimbali ikiwemo mabegi ya shule,sare za shule,kanga,kalamu,penseli na vitu vingine kadha wa kadha muhimu katika maisha yao.


Mwandishi wetu,Kadama Malunde ametuletea picha za matukio yaliyojiri kuanzia mwanzo hadi mwisho.Fuatilia hapa chini.


Hapa ni katika viwanja vya hoteli ya Lutheran Uhuru mjini Moshi ambapo hafla ya kufunga Ariel Camp 2016 imefanyika.Miongoni mwa wageni waliohudhuria katika kambi hiyo ni maafisa kutoka AGPAHI ,madaktari bingwa wa watoto,wataalaamu wa masuala ya kisaikolojia,Afisa Mradi Kitengo cha Tiba na Matunzo,Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Ukimwi Dr. Florence Ndaturu na Mratibu wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS) mkoa wa Kilimanjaro bi Razia Ngaina. 

Wengine ni bi Pamela Muro,ambaye ni mwakilishi kutoka shirika la Ndege la Precision Air lililosafirisha watoto na vijana kutoka Mwanza hadi Kilimanjaro pia Kilimanjaro kwenda Mwanza,mwakilishi Ofisi ya mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro bwana Paul Shayo na wasimamizi wa watoto kutoka vituo vya afya.
Watoto na vijana wa Ariel Camp 2016 wakiandamana kuelekea kwenye eneo la hafla ya kufunga kambi hiyo iliyodumu kwa muda wa siku tano mkoani Kilimanjaro.
 
Maandamano yanaendelea.
Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la AGPAHI, Dr. Sekela Mwakyusa aliyekuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo akipokea maandamano ya watoto na vijana. Dr. Mwakyusa pia ni rais wa Chama Cha Madaktari Bingwa wa Watoto Tanzania. Kulia ni Mratibu wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS) mkoa wa Kilimanjaro bi Razia Ngaina.
Vijana na watoto wakiandamana.
Meza kuu wakishuhudia maandamano ya watoto na vijana-Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la AGPAHI, Dr. Sekela Mwakyusa ,katikati ni Mratibu wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS) mkoa wa Kilimanjaro bi Razia Ngaina.Wa kwanza kulia ni Afisa Mradi Kitengo cha Tiba na Matunzo,Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Ukimwi Dr. Florence Ndaturu.

Watoto na vijana wakicheza na walezi wao kutoka mikoa ya Shinyanga na Simiyu.

Washiriki wa kambi wakiimba na kucheza.

Kila mmoja anacheza katika staili yake.

Walezi wa watoto na vijana wakionesha mbwembwe zao katika kucheza.

Meza kuu wakiangalia burudani iliyokuwa inaendelea.

Mwakilishi Ofisi ya mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro bwana Paul Shayo akizungumza katika hafla hiyo ya kufunga kambi ya 6 ya Ariel mwaka 2016.

Vijana na walezi wakiwa eneo la tukio.

Kushoto ni Mwakilishi Ofisi ya mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro bwana Paul Shayo akiwa na mkurugenzi wa shirika la AGPAHI, Dr. Sekela Mwakyusa.

Vijana wakifurahia jambo.

Tunafuatilia kinachoendelea hapa.....
Kushoto ni mshindi wa shindano la Miss Ariel mwaka 2016 akionesha pozi zake kwa mgeni rasmi,ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la AGPAHI, Dr. Sekela Mwakyusa (kulia).

Maafisa kutoka AGPAHI wakiteta jambona wengine wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea .

Afisa miradi huduma unganishi kwa jamii AGPAHI, Richard Kambarangwe akisoma historia ya klabu za watoto na kambi ya Ariel.Alisema shirika la AGPAHI lilianzisha huduma za kisaikolojiakwa watoto mwaka 2011,mpaka kufikia Juni mwaka 2016 kuna takribani klabu 50 zenye watoto takribani 2448 kutoka mikoa ya Shinyanga na Simiyu.

Kambarangwe alisema kupitia kambi za watoto za kila mwaka,AGPAHI huwakutanisha watoto wanachama wa klabu kutoka vituo mbalimbali,ambao hujifunza na kupata uzoefu kutoka kwa watoto wenzao, kupata elimu ya Afya na makuzi, kujifunza stadi za maisha, kupata huduma ya kisaikologia na Kiafya , kucheza, kuwapa watoto nafasi ya kuonyesha vipaji vyao na kutembelea maeneo mbalimbali ya kihistoria kuongeza ufahamu wao kuhusu jiografia ya Tanzania.

Washiriki wa kambi ya Ariel wakisikiliza historia ya klabu za kambi....Kambarangwe aliongeza kuwa AGPAHI haiishi tu kuhamasisha kuundwa kwa klabu za watoto na vijana bali watoto wamekuwa wakinufaika kwa kupata chakula na vinywaji angalu kwa kila mwezi wanapokutana kwenye klabu zao, pia wamewekewa vifaa vya kuchezea kama bembea,mipira, midori kwa watoto wadogo, baiskeli za watoto na vifaa vya kuchora kuonesha vipaji vyao, pia wamepata luninga na CD zenye kutoa mafunzo.

Afisa miradi huduma unganishi kwa jamii AGPAHI, Richard Kambarangwe akikabidhi taarifa kuhusu historia ya klabu na kambi za watoto kwa mgeni rasmi,Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la AGPAHI, Dr. Sekela Mwakyusa.
Afisa miradi huduma unganishi kwa jamii kutoka AGPAHI, Cecilia Yona akiwaribisha vijana kutoa ushuhuda jinsi walivyopata maambukizi ya VVU,wanavyopata tiba na matunzo lakini pia changamoto wanazopitia katika maisha yao na namna wanavyopata msaada kutoka shirika linalojali watoto na kukaa nao karibu ili waweze kuishi maisha yao yote na kufanikisha ndoto zao za kimaisha na wawe na matumaini chanya.
 
Mmoja wa vijana wa Ariel Camp 2016 akitoa ushuhuda jinsi alivyopata maambukizi ya VVU.

Washiriki wa Ariel Camp 2016 wakitafakari.

Kijana akitoa ushuhuda jinsi alivyopata maambukizi ya VVU na kuanza kutumia dawa kufubaza makali ya VVU.
Meza kuu wakitafakari ushuhuda wa vijana na watoto jinsi walivyopata maambukizi ya VVU na namna wanavyoishi kwa kuzingatia masharti ya kuwa wafuasi wazuri wa dawa.
Kijana akiimba wimbo wa kulipongeza shirika la AGPAHI kwa kujali watoto.

Wadau kutoka mashirika mbalimbali yanahusika na masuala ya watoto wasikiliza wimbo kutoka kwa vijana hao.

Vijana wakiimba wimbo.

Vijana wakiimba kwa hisia.

Kijana akitoa ushuhuda jinsi alivyopata maambukizi ya VVU kutoka kwa mama yake wakati wa kujifungua.

Kijana akisimulia jinsi anavyotumia dawa za kufubaza makali ya VVU tangu akiwa mdogo.

Kijana akitoa ushuhuda jinsi alivyopata maambukizi ya VVU.

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la AGPAHI, Dr. Sekela Mwakyusa akikata keki na washiriki wa kambi ya Ariel.Washiriki wote wa Ariel Camp walikula keki wakiongozwa na Dr. Mwakyusa.

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la AGPAHI, Dr. Sekela Mwakyusa akijiandaa kuwalisha keki watoto na vijana.

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la AGPAHI, Dr. Sekela Mwakyusa akimlisha keki mmoja wa vijana hao aliyeamua kupiga magoti akifuata mila na desturi za kabila la Kisukuma ambapo kupiga magoti huonesha kuwa anayepiga magoti ana maadili mema.

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la AGPAHI, Dr. Sekela Mwakyusa akimlisha keki Miss Ariel Camp mwaka 2016.

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la AGPAHI, Dr. Sekela Mwakyusa akijiandaa kumlisha keki Mr. Ariel Camp mwaka 2016.

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la AGPAHI, Dr. Sekela Mwakyusa akimlisha keki Mr. Ariel Camp mwaka 2016.

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la AGPAHI, Dr. Sekela Mwakyusa akimlisha keki Afisa miradi huduma unganishi kwa jamii AGPAHI, Richard Kambarangwe kwa niaba ya maafisa wote kutoka AGPAHI walioshiriki kambi hiyo.

Miss Ariel Camp 2016,akimlisha keki Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la AGPAHI, Dr. Sekela Mwakyusa.

Mr. Ariel Camp 2016,akimlisha keki Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la AGPAHI, Dr. Sekela Mwakyusa.

Mr. Ariel Camp 2016,akimlisha keki Mwakilishi Ofisi ya mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro bwana Paul Shayo

Vijana wakisoma risala kwa mgeni rasmi,ambapo pamoja na mambo mengine walilishukuru shirika la AGPAHI kwa kuwasaidia watoto kwa mambo mbalimbali.

Vijana hao pia walipaza kilio chao kwa serikali kuwajali zaidi watoto na kuyaomba mashirika mengine kujitokeza kusaidia watoto kwa vitendo.

Igizo likachukua nafasi yake.

Mgeni rasmi ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la AGPAHI, Dr. Sekela Mwakyusa akizungumza wakati wa kufunga kambi ya Ariel ambapo aliiomba serikali ya Tanzania kuendelea kushirikana shirika lake ambalo limekuwa msaada mkubwa kwa watanzania katika mapambano dhidi ya maambukizi ya VVU na Ukimwi.

Dr. Mwakyusa akizungumza wakati wa kufunga kambi ya Ariel mwaka 2016.

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la AGPAHI, Dr. Sekela Mwakyusa akisisitiza jambo.

Muda wa zawadi kwa watoto, vijana na walezi ukawadia.

Mabegi ya shule yakiwa na kalamu,madaftari,penseli,soksi na kanga yakiwa tayari kugawiwa kwa watoto na vijana.

Meneja Mawasiliano na Huduma za Jamii kutoka AGPAHI, Jane Shuma akitoa maelekezo kuhusu zoezi la utoaji zawadi. Alisema mabegi hayo ya shule yana peni, penseli, madaftari,soksi na kanga na kuongeza kuwa wakati wa wiki ya kambi washiriki walipewa sare za shule na viatu.

Meneja Mawasiliano na Huduma za Jamii kutoka AGPAHI, Jane Shuma akionesha moja ya mabegi hayo ya kisasa kwa ajili ya washiriki wa Ariel Camp mwaka 2016.

Afisa miradi huduma unganishi kwa jamii AGPAHI, Richard Kambarangwe akionesha mfano wa madaftari yaliyomo katika kila begi.

Afisa miradi huduma unganishi kwa jamii AGPAHI, Richard Kambarangwe akionesha mfano wa kanga zilizomo katika kila begi.

Dr. Mwakyusa akimkabidhi begi mmoja wa watoto

Zoezi la kukabidhi zawadi linaendelea.

Dr. Mwakyusa akishikana mkono na mtoto wakati akimkabidhi begi la shule.

Dr. Mwakyusa akishikana mkono na kumkabidhi zawadi ya cheti mlezi wa watoto kutoka zahanati ya Kagongwa halmashauri ya Mji Kahama mkoa wa Shinyanga Emelda Ndunguru.

Mlezi wa watoto kutoka wilaya ya Ushetu mkoani Shinyanga, Nuru Jackson akipokea zawadi.

Muuguzi mkunga kutoka zahanati ya Old Shinyanga,ambaye ni mlezi wa watoto katika zahanati hiyo, Anaschola Ndigawe akipokea zawadi.
Mlezi wa watoto kituo zahanati ya Old Shinyanga katika manispaa ya Shinyanga Anaschola Ndigawe akiwa amebeba zawadi zake.Muuguzi huyu maarufu kwa jina la "MC Mama Sabuni "ndiye alikuwa mshereheshaji mkuu katika hafla ya kufunga Ariel Camp 2016.

Meneja Mawasiliano na Huduma za Jamii kutoka AGPAHI, Jane Shuma akizungumza wakati mwakilishi kutoka Shirika la Ndege la Precision Air, Pamela Muro (kushoto mwenye miwani) akikabidhiwa zawadi ya cheti cha shukrani.

Mwakilishi wa Lutheran Uhuru Hotel,bwana Nelson Munisi ambapo ndipo watoto,vijana na walezi walikuwa wanapata huduma zote za kimwili kwa muda wote wakiwa kambini akipokea zawadi ya cheti.

Afisa kutoka AGPAHI bwana Felix Muchira akitoa zawadi kwa washiriki wa kambi hiyo,akiwemo mtunza muda wakati wa kambi.

 
Waruka sarakasi kutoka kundi la Kilimanjaro Arts Academy wakionesha vipaji vyao.
 
Waruka sarakasi wakionesha mbwembwe zao.

Picha ya pamoja wafanyakazi wa shirika la AGPAHI na wageni waalikwa.
Picha ya pamoja wafanyakazi wa shirika la AGPAHI,wageni waalikwa na washiriki wa kambi kutoka mashirika mbalimbali.

Picha ya pamoja wafanyakazi wa shirika la AGPAHI,wageni waalikwa,watoto na washiriki wa kambi kutoka mashirika mbalimbali yanayohusika na masuala ya watoto.
Picha ya pamoja wafanyakazi wa shirika la AGPAHI,wageni waalikwa na vijana.
Picha ya pamoja wafanyakazi wa shirika la AGPAHI,wageni waalikwa na vijana.

Picha ya pamoja wafanyakazi wa shirika la AGPAHI,wageni waalikwa na walezi wa watoto.

Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog

Bofya <<HAPA>> kuangalia Picha Watoto na Vijana wa Ariel Camp Wakifanya Utalii Mkoani Kilimanjaro 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com