Kesi inayomkabili Isaac Abakuk ambaye anatuhumiwa kumtukana Rais John Magufuli kwenye ukurasa wake wa facebook jana June 07 2016 ilishindwa kuendelea kutokana na upande wa Jamhuri kutokamilisha ushahidi na kuiomba Mahakama kuahirisha shauri hilo hadi leo June 08 2016.
Hakimu anayesikiliza kesi hiyo Augustine Rwezire wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha alikubali ombi hilo na kuahirisha kesi hiyo ambapo inatarajiwa kuanza kusikilizwa mfululizo. Mshtakiwa anaendelea kuwa nje kwa dhamana kusubiri kesi yake itakapotajwa.
Social Plugin