Mti wa ajabu aina ya Muembe umewavuta mamia ya wakazi wa Tengamano Jijini Tanga kuushuhudia ambapo inadaiwa kuwa mwembe huo ikifika majira ya jioni hubadilika na kuwa na taswira ya mwalimu Nyerere kwa upande mmoja na Mama Maria Nyerere kwa upande wa pili.
Tukio hilo limesemekana lilianza kujitokeza June 6 2016. "Ni kama muujiza fulani sio kwamba jambo hili liliwahi kujitokeza, hapa nilipo ndio naona hali halisi ya huu mwembe, ni kama mtu alijaribu kuuchonga"- Anasimulia shuhuda wa Tukio hilo Awadhi Ally
Social Plugin