MRADI
wa Mabasi Yaendayo Haraka jijini Dar es Salaam (UDART) imeanzisha
huduma kwa wateja wao za kutumia kadi maalumu wakati wa kupanda mabasi
hayo itakayoanza rasmi leo.
Akizungumza
na waandishi wa habari Dar es Salaam jana asubuhi, Mkurugenzi Mtendaji
wa UDART, David Mgwasa alisema wameanza kutoa huduma hiyo ya kadi ili
kuwarahisishia wateja wao na kuondoa changamoto ya kusubiri tiketi kwa
muda mrefu kabla ya kuondoka.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Kampuni ya MaxMalipo ambao wameingia ubia na Udart katika
matumizi ya kadi hizo, Mhandisi Juma Rajabu alisema kwamba kwa kuanzia
wametoa kadi 200,000 ambapo kila kadi itauzwa kwa shilingi 5000 ingawa
bei halisi kwa kadi moja ni shilingi 500 na sh.4500 inayobaki itakuwa ni
malipo ya mteja wao.
"Shilingi
4500 zitatumika kama malipo ya nauli kwa siku saba hadi nane kwa kwenda
eneo lolote na kuwa kadi hizo zitapatikana katika vituo vya Kimara,
Mbezi, Morocco, Gerezani, Posta na kuwa zitakuwa ni endelevu" alisema Rajabu.
Aliongeza
kuwa katika nchi nyingi zimekuwa zikitumia kadi hizo katika kusafirisha
abiria na kuwa kwa hapa nchini ni huduma mpya ambayo itakuwa na
changamoto zake kabla ya kuzoeleka.
Alisema
licha ya kuanzisha huduma ya kadi bado ile ya risiti itaendelea kama
kawaida ambapo alisema namna ya kujiunga na huduma hiyo unatakiwa kupiga
*152*22#.
Social Plugin