Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

Mbunge Joseph Mbilinyi Maarufu Sugu Kikaangoni kwa Kuwaonyeshea Kidole Cha Kati Wabunge wa CCM


Naibu Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson ameitaka Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kuchunguza tuhuma dhidi ya Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi maarufu Sugu anayedaiwa kuwaonyeshea kidole cha kati wabunge wa CCM.


Sugu anadaiwa kufanya kitendo hicho June 6, mwaka huu alipokuwa akitoka katika ukumbi wa Bunge baada ya kuwasilisha maoni ya kambi ya upinzani kuhusu azimio la bunge kuridhia mkataba wa kimataifa wa udhibiti wa matumizi ya dawa na mbinu za kuongeza nguvu michezoni.


Naibu Spika ameitaka kamati hiyo kumchukulia hatua kali kama watamkuta na hatia ya kufanya kitendo hicho

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com