Mfanyabiashara huyo baada ya tukio alimpeleka Grace Wangechi Kinyanjui hospitalini akidai kajipiga risasi mwenyewe na Kinyanjui alifariki muda mfupi baadae kutokana na majeraha makubwa aliyoyapata. Mtuhumiwa amefikishwa mahakamani na ataendelea kushikiliwa siku tano zaidi wakati polisi wakiendelea na uchunguzi.
Kamanda wa polisi Japheth Koome amesema wanandoa hao wamekuwa kwenye mahusiano na walikuwa wanaishi pamoja pia majeraha ya Kinyanjui yanaendana na mauaji na kulikuwa na jeraha la risasi nyuma ya kichwa chake pia alikuwa na majeraha matatu upande wa kushoto wa shingo yake.
Grace Wangechi Kinyanjui wakati wa uhai wake
Social Plugin