Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

Rais Magufuli Apokea Ripoti ya Uchaguzi 2015,Airudishia NEC Bilioni 12 Kujengea Ofisi



Rais wa Tanzania Dokta.John Pombe Magufuli amesema kuwa yupo pamoja na wanasiasa na atashirikiana nao vyema kwa kupokea ushauri,Maoni walio nayo kwa mikono miwili kwa kuwa ameamua kufanya kazi na vyama vyote vya siasa ili kuhakikisha kuwa anatatua kero zilizopo katika taifa. 
 
 
Amesema hayo wakati akikabidhiwa Ripoti ya Uchaguzi mkuu wa Mwaka jana 2015 Ikulu jijini Dar es Salaam, huku akisisitiza kuwa Uchaguzi umeisha na hakuna aliyeshinda wala aliyeshindwa watanzania wote wameshinda hivyo ni muda wa kuhakikisha nchi inasonga mbele. 
 

Awali Kabla ya kumkabidhi Rais Ripoti ya Uchaguzi ya Mwaka jana 2015 ,Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi NEC Jaji Damiani Lubuva alibainisha mambo kadhaa ambayo yamekuwa yakiwakabili wakati wa mchakato mzima wa uchaguzi kuwa ni kutokuwepo kwa jengo lake kwaajili ya shughuli hizo jambo lililofanya wawe wakipoteza fedha nyingi kulipia pango la ofisi hizo. 
 

Kufuatia Changamoto hizo Rais Magufuli amelazimika kuzirudisha fedha ambazo alikabidhiwa na Tume hiyo kama kiasi kilicho baki wakati wa uchaguzi wa Mwaka 2015 na kuitaka Tume hiyo itumie fedha hizo Shilingi Bilioni 12 kwa ajili ya kutengeneza Ofisi ya Jengo lake lenyewe. 
 

Rais Magufuli amekiri wazi kwa Tume hiyo kuotokuwa na jengo lake na kusema kuwa itapendeza mno endapo NEC itazijenga ofisi hizo Mkoani Dodoma kama moja ya njia ya kumuenzi Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ambaye alisema Dodoma Makao Makuu ya Tanzania. 
 

"Mimi mwenyewe nilishuhudia ukubwa wa changamoto hii ya kukosa jengo la ofisi hizi za tume (NEC) wakati nilipoenda kuchukua fomu za nakiri kwa dhati ofisi ya tume ilipo sio muafaka na ipo kwenye jengo la kupanga",alisema.
 

Pia ameipongeza tume ya Uchaguzi NEC kwa kusimamia vyema uchaguzi wa mwaka jana na kusema kuwa suala la uchaguzi ni tukio muhimu mno katika nchi kwani niwazi kuwa suala hilo huleta migogoro katika nchi, huku akitolea mfano baadhi ya nchi ambazo zimeingia kwenye migogoro na machafuko kutokana na masuala hayo ya uchaguzi na kukuta yakigharimu maisha ya wananchi wake. 
 

Amekiri kuwa Uchaguzi wa mwaka jana ulikuwa wenye ushindani mkali,na uliokuwa na mvuto wa kipekee ndani na nje ya nchi licha ya kuwa kwamba ni mara ya kwanza kutumia mfumo wa BVR katika mchakato huo. 
 

Hata hivyo kwa upande wa Mwenyekiti wa NEC Jaji Damiani Lubuva ameongeza kwa kusema kuwa kama tume watahakikisha kuwa mapungufu yaliyojitokeza kwenye uchaguzi uliopita watajitahidi kuyaboresha zaidi katika chaguzi ujao.
Via>>ITV

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com