Serikali imeiagiza ofisi ya mkemia mkuu kutoa haraka majibu ya sampuli za vipimo vilivyochukuliwa kwa majeruhi wa ugonjwa wa ajabu uliozuka mkoani Dodoma na kusababisha vifo vya watu saba huku wengine 21 wakilazwa kwani kuchelewa kutoa majibu hayo kunasababisha hofu kuzidi kutanda sambamba na kuzua mihemuko kwa wakazi wa maeneo yaliyokubwa na ugonjwa huo.
Waziri wa afya maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto Ummy Mwalimu ametoa agizo hilo alipotembelea kijiji cha Mwakisabe kilichopo wilayani Chemba kinachodaiwa kuwa kiini cha kuibuka ugonjwa huo wa ajabu ambapo amesema kuchelewesha majibu ya vipimo vya sampuli kunaibua hisia tofauti kwa wakazi wa maeneo hayo ambapo sasa unahusishwa na imani potofu hali inayoweza kuhatarisha amani.
Katika ziara hiyo waziri Mwalimu amekutana na baadhi ya watu waliokula nyama ya Ng’ombe anayedaiwa anayesemekana ndiyo chanzo cha ugonjwa hu.
Kwa upande wake mbunge wa jimbo la Chemba Juma Nkamia ameshangazwa na tukio hilo ambalo linazidi kuleta sintofahamu kwa wakazi wa wilaya za Kondoa na Chemba huku mganga mkuu wa mkoa wa Dodoma Dk James Charles akikanusha ugonjwa huo kuhusishwa na nyama kwani baadhi ya watu wamegundulika baadhi yao kutokula nyama hiyo.
Via>>ITV
Social Plugin