Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

Ubeligiji Wamejenga Bomba la Kusafirisha Bia, Wateja Watapata Bia Moja Kila Siku,Tazama Video

Xavier Vanneste kutoka Ubeligiji alipata wazo la kujenga bomba litakalosafirisha bia miaka minne iliyopita, mwanzoni lilionekana wazo lisiloeleweka, lakini baadae likakubalika na takribani wanywaji 400 wakajitokeza kuchangia mradi huo.



Xavier Vanneste

mmoja wa watu waliochangia mradi huo ambaye ni mmiliki wa mgahawa, Philippe Le Loup anasema………."Inatakiwa uwe kama una kichaa fulani kidogo hivi kama bia yenyewe kufanya mradi kama huu, mimi nilikuwa na pesa kwa ajili hiyo kwa hiyo nikapenda nikatoa fedha".

Katika mradi huu wanywaji walichangisha dola milioni 3 hivyo wameahidiwa kupata bia moja kila siku bure maisha yao yote.

Xavier Vanneste amekuja na wazo la kutengeneza bomba kwa ajili ya kusafirisha bia kwa sababu hakutaka kutumia malori kwa kuwa yangeharibu mji, bomba limetoka ilipo kampuni ya bia kuelekea nje ya mji kama km 2.


Malori yaliyokuwa yakitumika kabla

Unaweza kuangalia video hii hapa chini

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com