Moja ya stori kwenye gazeti la Jambo Leo ,leo Jumatatu ni stori yenye kichwa cha habari ‘Watanzania milioni 39 wanakunywa mataputapu’
Gazeti hilo limechapisha utafiti uliofanywa na shirika la Afya Dunia ‘WHO’ umeonesha kuwa 87% ya watanzania wanakunywa pombe za kienyeji, huku mikoa ya Dar es salaam na Kilimanjaro ikiiongoza kwa kuwa na wanywaji wengi wa pombe hiyo.
Mkoani Kilimanjaro eneo linaloongoza kwa wanywaji wa pombe hiyo ni Moshi, kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012 Tanzania ilikuwa na watu wanaokadiriwa kuwa zaidi ya milioni 44.9, hivyo 87% ya idadi hiyo kulingana na utafiti huo ni watu milioni 39.06.
Kulingana na gazeti la Jambo Leo limeeleza kuwa utafiti huo umebaini kuwa kwa sasa vijana wengi wanatumia pombe kupita kiasi kuanzia shule ya msingi hadi vyuo vikuu hali inayosababisha wakumbwe na magonjwa ya akili na kujiingiza kwenye vitendo vya uhalifu.
Matokeo ya utafiti huo yalitangazwa jana katibu mkuu wa chama cha wataalam wa afya ya akili Tanzania (MEHATA), Dk. Kissah Mwambene.
Alikuwa akitoa mada kwa wabunge juu ya athari za matumizi za matumizi ya pombe iliyoandaliwa na chama cha waandishi wa habari wanawake ‘TAMWA’.