Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

UWT Shinyanga Vijijini Watoa Tamko Kuhusu Rais Magufuli,Wachangia Damu ,Tazama Picha 22


 
Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT) wilaya ya Shinyanga vijijini umempongeza rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli kwa kuimarisha na kujenga upya misingi ya uongozi na uwajibikaji iliyoanzishwa na baba wa taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere hali iliyosababisha wananchi kuwa na imani na serikali yao.

Hayo yamesemwa jana na katibu wa UWT wilaya ya Shinyanga Vijijini Grace Haule katika kikao chao kilichofanyika katika ukumbi wa NSSF mjini Shinyanga wakati akitoa tamko la UWT wilaya hiyo kwa rais Magufuli na makamu wa rais Samia Suluhu kwa kuchaguliwa na kwa utekelezaji mzuri wa kazi zao tangu kuchaguliwa kwao katika uchaguzi mkuu uliopita.


Haule alisema umoja huo unampongeza rais Magufuli na makamu wa rais kwa kazi kubwa wanayofanya ya kuijengea heshima nchi tangu walipochagulia hali iliyosababisha nchi na Chama Cha Mapinduzi kujipatia heshima kubwa.


“Rais Magufuli ameijengea heshima kubwa nchi yetu kwa kuimarisha na kujenga upya misingi ya uongozi na uwajibikaji iliyoanzishwa na baba wa taifa Mwalimu Julius Kambarage,hali hii imewafanya wananchi kuwa na imani na serikali yao kwa ajili ya kuwaletea maendeleo katika Nyanja zote”,alieleza Haule.


Aidha Katibu huyo wa UWT,alisema kuwa wanatoa pongezi kwa hotuba nzuri ya kwanza ya rais Magufuli aliyoitoa yenye kuonesha malengo,kuthubutu,jitihada na mwelekeo na dira ya serikali ya awamu ya tano aliyoitoa wakati wa akihutubia bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tarehe 20.11.2015.

Haule alisema UWT wilaya ya Shinyanga Vijijini imeridhishwa na utaratibu wa rais Magufuli katika nidhamu ya matumizi ya fedha pia kupambana na mafisadi wakiwemo wala rushwa kazi ambayo ni kubwa na ngumu lakini kwa hatua aliyofikia inatia matumaini makuwa kwa wana CCM na Watanzania kwa ujumla.


“Kutokana na utendaji wa mheshimiwa rais akishirikiana na makamu wa rais na watendaji mbalimbali wa serikali nchi mbalimbali zimejenga imani kubwa kwa nchi yetu”,aliongeza Haule.

Kwa upande wake mgeni rasmi katika kikao hicho,kaimu katibu wa CCM mkoa wa Shinyanga Solomon Itunde aliwataka wanachama wa CCM kuhakikisha wanakuwa makini katika uchaguzi wa viongozi wa CCM mwaka 2017 ili kupata ushindi mnono katika uchaguzi mkuu 2020.

“Tukichagua viongozi sahihi katika uchaguzi wa ndani ya CCM mwaka ujao,itatusaidia kushinda uchaguzi mkuu 2020 kwa urahisi zaidi kwani viongozi hao watapigania maslahi ya chama kwa nguvu zao zote”,alieleza Itunde.


Hata hivyo Itunde aliwapongeza wanawake wa CCM wilaya ya Shinyanga Vijijini kwa kusimama kidete katika uchaguzi mkuu uliopita hali iliyosababisha kata zote 26 za wilaya hiyo kuchukuliwa na CCM huku kiti cha Ubunge jimbo la Solwa nacho kikichukuliwa na mgombea wa CCM Ahmed Salum.

Mbali na kujadili mambo kadha wa kadha ya kujenga Chama,
UWT wilaya ya Shinyanga vijijini wamechangia utoaji wa damu kwenye hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Shinyanga kwa lengo la kuondoa vifo vya mama na mtoto vitokanavyo na uzazi sababu ya kukosa wa damu.

Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Shinyanga inakabiliwa na tatizo la uhaba wa damu kwani kila siku hutumia uniti 20, kwa wiki uniti 150 hali ambayo ni hatari hususani kwa akina mama wajawazito na watoto ambao ndiyo wahitaji wakubwa wa damu hiyo.

Kaimu mratibu wa damu mkoa wa Shinyanga Felix Manda aliupongeza umoja huo wa wanawake wa (CCM) Kwa moyo waliouonyesha wa kuchangia damu, ikiwa hospitali hiyo inakabiliwa na tatizo hilo kwa asilimia kubwa ambapo inatakiwa kwa wastani kuwe na Uniti 150 kwa wiki.


Mwandishi wetu Kadama Malunde alikuwepo katika kikao hicho,ametuletea Picha 22 wakati wa kutoa tamko hilo na akina mama wa UWT wakichangia damu kwa ajili ya kuokoa maisha ya akina mama wajawazito na watoto..Tazama hapa chini
Hapa ni katika ukumbi wa NSSF mjini Shinyanga ambapo jana Juni 08,2016,Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT) wilaya ya Shinyanga vijijini umefanya kikao na kutoa tamko la kumpongeza rais John Pombe Magufuli kwa uongozi wake tangu achaguliwe mwaka 2015.Wa kwanza kushoto ni mwenyekiti wa UWT wilaya ya Shinyanga Vijijini Helena Daudi,akifuatiwa na kaimu katibu wa CCM mkoa wa Shinyanga Solomon Itunde,wa pili kutoka kulia ni kaimu katibu wa CCM wilaya ya Shinyanga Vijijini Denis Mayunga,wa kwanza kulia ni katibu wa UWT wilaya ya Shinyanga Vijijini Grace Haule
Mwenyekiti wa UWT wilaya ya Shinyanga Vijijini Helena Daudi akifungua kikao hicho
Katibu wa UWT wilaya ya Shinyanga Vijijini Grace Haule akitoa tamko la UWT wilaya hiyo kwa rais Magufuli na makamu wa rais Samia Suluhu kwa kuchaguliwa na kwa utekelezaji mzuri wa kazi zao tangu kuchaguliwa kwao katika uchaguzi mkuu uliopita.
Wajumbe wa UWT wilaya ya Shinyanga Vijijini wakiwa ukumbini
Katibu wa UWT wilaya ya Shinyanga Vijijini Grace Haule akitoa tamko la UWT wilaya hiyo
Wajumbe wa UWT wakiwa katika ukumbi wa NSSF mjini Shinyanga wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea katika kikao
Kikao kinaendelea
Katibu wa UWT wilaya ya Shinyanga Vijijini Grace Haule akizungumza ukumbiniWajumbe wa UWT Wilaya ya Shinyanga Vijijini wakiwa ukumbini

Aliyesimama ni mjumbe wa UWT taifa Dr. Christina Mzava akizungumza katika kikao hicho
Mgeni rasmi katika kikao hicho,kaimu katibu wa CCM mkoa wa Shinyanga Solomon Itunde akizungumza katika kikao hicho
Wajumbe wa UWT wilaya ya Shinyanga Vijijini wakifuatilia kilichokuwa kinajiri ukumbini
Kaimu katibu wa CCM mkoa wa Shinyanga Solomon Itunde akisisitiza jambo katika kikao hicho
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akizungumza katika kikao hicho ambapo aliwasisitiza akina mama kujenga urafiki na watoto wao na kuwapa elimu ya afya uzazi na kuwataka kuwasimamia watoto wa kike wasikatishwe masomo kwa kuolewa.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro alitumia fursa hiyo pia kuwasisitiza akina mama kujishughulisha na shughuli za maendeleo na kuhakikisha wanafichua watu wote wanaojihusisha na uhalifu katika jamii ikiwemo kuua vikongwe
Wajumbe wa UWT wilaya ya Shinyanga Vijijini wakijiandaa kuchangia damu nje ya ukumbi wa NSSF mjini Shinyanga
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akichangia damu
Katibu wa UWT wilaya ya Shinyanga Vijijini Grace Haule akichangia damu

Katibu wa UWT wilaya ya Shinyanga Vijijini Grace Haule akichangia damu
Mtaalam wa afya kutoka hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga akichukua taarifa muhimu kutoka kwa akina mama kabla ya kutoa damuKaimu mratibu wa damu mkoa wa Shinyanga Felix Manda akiandika maelezo kutoka kwa mmoja wa akina mama hao kabla ya kuchangia damu
Wanawake wa UWT wilaya ya Shinyanga Vijijini wakichangia damu-Picha zote na Kadama Malunde- Malunde1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com