Viongozi na makada wa Chadema waliokuwa wakisafiri kutoka Kahama kuelekea jijini Mwanza jana wamejikuta wakishindwa kuingia kwenye ofisi za chama hicho mjini Shinyanga kutia saini kitabu cha wageni baada ya Jeshi la Polisi kuzuia shughuli yoyote ya chama hicho mjini humo.
Waliokumbwa na adha hiyo ni pamoja na Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema, Freeman Mbowe, Katibu Mkuu, Dk Vicent Mashinji na wabunge Godbless Lema, Ester Bulaya, John Heche, Halima Mdee na viongozi kadhaa wa kitaifa wa Chadema.
Magari manne ya polisi yaliyosheheni askari waliobeba silaha na mabomu ya kutoa machozi yaliupokea msafara wa Chadema uliokuwa ukielekea Mwanza, mara tu ulipoingia mjini Shinyanga na kuusindikiza hadi nje ya mji kuhakikisha hausimami ndani ya mji huo.
Social Plugin