Mbunge wa Viti Maalumu, Munira Mustafa Khatibu (CCM) ameiomba serikali kukifuta Chama cha Wananchi (CUF) kutokana na kuhusika na vurugu Pemba.
Akijibu swali la Munira kuhusu kufuta chama cha CUF kwa madai kuwa kinachochea machafuko hayo, Naibu Waziri alisema jambo hilo liko mikononi mwa Msajili wa Vyama vya Siasa ambaye anatakiwa kuangalia mihemuko hiyo ya kisiasa.
Swali la Munira lilisababisha Mbunge wa Mwibara, Kangi Lugola (CCM), kuomba Mwongozo na kusema, “Mheshimiwa Naibu Spika nalazimika kuomba Mwongozo huu, kuna wakati naamini serikali yetu ikiwajibika kwa pamoja na Msajili wa Vyama vya Siasa hayumo humu ndani ambaye tunaamini ni sehemu ya serikali.”
Naibu Spika, Tulia Ackson, alitolea ufafanuzi kuwa kufutiwa usajili kwa CUF kutatokana na wanachama wake kufanya vitendo visivyofaa na kuathiri maisha ya watu na mali zao.
Masauni alisema kuwa maisha ya watu wa Pemba yamekuwa ya hofu wakati wote na hasa inapotokea kipindi cha uchaguzi kuisha na kusisitiza kuwa serikali imedhamiria kushughulikia jambo hilo.