Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

Wachungaji wa PPFT Waiomba Serikali Kufuta Usajili wa Kanisa la Askofu Gwajima




Askofu Josephat Gwajima
Ushirika wa wachungaji wa Kanisa la Kipentekoste Tanzania (PPFT) umeiomba serikali ifute usajili wa Kanisa la Ufufuo wa uzima la Askofu Josephat Gwajima kwa kukiuka maadili ya kanisa kwa kutoa kauli za uchochezi na kuzisambaza kwenye mitandao ya kijamii. 
 
 
Mwenyekiti wa ushirika wa wachungaji hao Askofu Pius Ikongo mwenye makao yake katika Halmashauri ya wilaya ya Mwanga mkoani Kilimanjaro amesema,kauli hizo zinaweza kubadili fikra za wananchi na kuzaa chuki dhidi ya serikali yao na kusababisha vurugu na uvunjifu wa amani.

Askofu Ikongo ametoa tamko hilo katika taarifa yake kwa vyombo vya habari na kueleza kuwa kitendo kilichofanywa na Askofu Gwajima kinapaswa kulaaniwa na wapenda amani wote waliopo ndani na nje ya nchi.

Mwenyekiti huyo wa PPFT amesema, kosa kubwa ambalo limewaumiza wachungaji wa Kipentekoste ni kitendo cha Askofu Gwajima kutumia Kanisa kama jukwaa la kisiasa kwa kuleta uchonganishi kati ya serikali ya awamu ya nne na iliyopo madarakani.
Via>>ITV

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com