Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

Wakili Apigwa na Kuchaniwa Nguo Mahakamani



Wakili wa China aliyevuliwa nguo

Mawakili wengi wa China wamenyanyaswa,kukamatwa na hata kufungwa jela lakini picha ya mmoja wao aliyekuwa na nguo zake zilizovuliwa na maafisa wa polisi imevutia hisia nyingi nchini China.

Wu Liangshu alikuwa katika mahakama ya wilaya ya Qingxiu akiwa amevalia koti lake na suruali ya ndani ikionekana.

Yeye na mawakili wengine waliambia maafisa wa mahakama kwamba alishambuliwa na maafisa watatu wa polisi katika mahakama moja mbele ya majaji mawili ambao walikataa ombi lake la kutaka kuanzisha kesi katika mahakama ya wilaya ya Nanning Mkoani Guangxi.

Bw Wu alipewa nguo nyingine lakini alijua uwezo wa kile alichokuwa akipanga kukifanya.''Asante alisema''.

Wakili huyo baadaye alitembea kupitia mlango wa mbele akiwa amebeba nakala zake za mahakamani akiwa na kalamu iliowekwa katika mfuko wa shati liliposuliwa.

Baadaye alipigwa picha nje ya jengo hilo la mahakama.


Chanzo-BBC

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com