Jeshi la Burundi limewasimamisha masomo Wanafunzi wa darasa la nane baada ya kuzichorachora vibaya picha za raisi wa Burundi Pierre Nkurunziza ambapo waliosimamishwa ni zaidi ya 300 ambapo pamoja na kuzichorachora, wameziharibu kwa makusudi.
Wanafunzi wa shule hiyo iliyopo Ruziba kusini mwa mji mkuu wa Bunjumbura wamesimamishwa baada ya Mfanyakazi wa shule hiyo kukuta vitabu vya kusomea vikiwa na picha za rais huyo zikiwa zimechorwa vibaya na maneno ya kashfa na matusi yakiwa yameandikwa.
Utawala wa shule hiyo umethibitisha kwamba ni zaidi ya vitabu 4o vimechafuliwa na kwamba mikakati ya kumaliza swala hilo imepatikana na kuafikiwa lakini bado hakutaja chochote kuhusu kurudi kwa wanafunzi hao shuleni.
Rais huyu wa Burundi toka ametangaza kuwania muhula wa tatu kuiongoza Burundi kumetokea machafuko na watu kuuwawa huku wengi wao wakionekana kumpinga na kutotaka asiendelee kuwepo madarakani.
Social Plugin