Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

Watoto Sita Wafariki Wakibatizwa Mtoni Huko Zimbabwe


NB-Siyo picha katika  habari hapa chini

Watoto sita wamekufa maji bila kutarajiwa katika sherehe za kubatizwa kwao katika mto nchini Zimbabwe.
 
Watoto watatu walinusurika kufa maji ya mto huo ambao maji yake ni ya baridi.
 
Watoto hao walionekana wakitetemeka kutokana na baridi wakati miili ya wenzao waliokufa maji ikiopolewa majini.

Polisi nchini Zimbabwe wamewatia mbaroni watu wawili ambao ni wafuasi wa dhehebu hilo la Kikristo.

Lakini pia walimjumuisha mama mmoja ambaye alidai kwamba yeye ni nabii ambaye alisema kwamba alifanya jaribio la kufufua wafu wakati wa ibada zake .

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com