Watuhumiwa 711 Wakamatwa Ndani ya Siku 4 Jijini Dar es Salaam


Kamanda wa polisi kanda maalumu Dar es salaam Simon  Sirro amesema jumla ya watuhumiwa 711 wa makosa tofauti tofauti wamekamatwa kati ya siku ya Juma tatu mpaka Alhamisi usiku wiki hii.


Akitoa taarifa kwa wanahabari leo  Kamanda Sirro amesema kuwa watuhumiwa hao walikamatwa kwa makosa mbalimbali yakiwemo ya unyang’anyi wa kutumia nguvu, kukutwa na bhangi na gongo kucheza kamari,biashara za kuuza mwili pamoja na kubugudhi abiria.


Aidha kamanda Sirro amewataka wenyeviti wa mitaa kuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha kwamba maeneo yanayowazunguka yanakuwa shwari kwa kuhakikisha hakuna biashara haramu zinazoendelea za kusababisha uhalifu.


Hata hivyo ametaja maeneo yanayoongoza kwa kuwa na wauzaji wa bangi na gongo katika maeneo ya Dar es salaam ni Kawe na Mabibo na kueleza kuwa operesheni maalumu itaendelea kufanyika kila siku kuhakikisha mitaa inakuwa safi.


Ameongeza kwamba kwa sasa pia vijana wajulikanao kama panya road nane wamekamatwa na kudai kuwa wanatumiwa kufanya matendo ya ki uhalifu na tajiri mfanyabiashara wa kariakoo jijini Dar es salaam.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post