Waziri Mkuu wa Uingereza Ajiuzulu,Mgombea Urais Nchini Marekani Donald Trump Achekelea

Waziri mkuu wa Uingereza, David Cameron, ametangaza atajiuzulu, baada ya kushindwa kuwashawishi raia wengi wa Uingereza, kusalia katika muungano wa Ulaya.


Cameron akiwa amejawa na huzuni amesema kuwa atasalia ofisini kwa siku tisini zijayo ndipo angatuke.



Bw Cameron ambaye ameongoza kampeini ya kusalia katika muungano wa EU amesema kauli hiyo imempa mshutuko mkubwa na kwa baadhi ya watu mashuhuri duniani.

Akiongea katika kikao cha waandishi wa habari nje ya afisi yake jijini London, Bwana Cameron amesema kuwa hahisi tena kuwa mtu muhimu wa kuliongoza taifa hilo kwa ufanisi chini ya uamuzi kama uliofanywa.



Sauti yake iliibua hisia hasa aliposena naipenda saana taifa hili na najihisi vizuri kuliongoza muda huo wote.

Bwana Cameron amesema kuwa kauli ya wengi sharti isikizwe japo hafahamu kwanini Waingereza walichukua uamuzi kama huo ilhali taifa hilo lilikuwa linaufanisi mkubwa sana ndani ya EU.

Cameron akiwa ameandamana na mkewe amesema bila shaka sasa utawala mpya unahitajika utakaoweza kutathmini mbinu na mkataba wa kujiondoa kutoka kwa muungano huo wa bara Ulaya.



Donald Trump
Wakati huo huo Mgombea kiti cha urais nchini Marekani Donald Trump amepongeza hatua ya raia wa Uingereza kujiondoa katika muungano wa Ulaya akisema "wamekomboa nchi yao".

Amesema hayo alipowasili Trump Turnberry kwa ufunguzi wa mgahawa wa Ayrshire na ukumbi wa gofu,baada ya kufanyiwa ukarabati.

Kuna madai kuwa alinunua Hoteli hiyo kwa kima cha pesa ambazo hazikutajwa mwaka 2014.

Ufungamano wa kibiashara baina ya Scotland na bilionea huyo wa Marekani ulianza muongo mmoja uliopita alipoahidi kudumisha urithi wa mamake Mary MacLeod, aliyezaliwa Stornoway mwendo mfupi kutoka eneo la Hebrides.

Bwana Trump ambaye anasifika kwa kumiliki hoteli nyingi za kifahari pamoja na nyanja za gofu nchini Marekani pia alifungua moja ya Hoteli hizo nchini Uingereza katika jimbo la Menie mjini Aberdeenshire,mwaka 2012 baada ya mzozo juu ya mipango na masuala ya mazingira ambayo yalipingwa na wenyeji waliokataa kuhama.

Maandamano dhidi mgombea huyo wa urais wa Marekani wa chama cha Republican yanatarajiwa, kutoka kwa wale wanaomlaumu kwa ubaguzi wa rangi.
Via>>BBC

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post