Juni 28,2016 klabu ya Dar es Salaam Young Africans ilirejea katika uwanja wa Taifa Dar es Salaam ambao ndio uwanja inaoutumia kama uwanja wake wa nyumbani kucheza mechi yake ya pili hatua ya nane bora dhidi ya klabu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Katika mchezo huo wa Kundi A lenye timu za Medeama ya Ghana, Mo Bejaia ya Algeria, TP Mazembe ya Kongo na Yanga, umemalizika kwa Yanga kupoteza kwa goli 1-0, goli ambalo limefungwa dakika ya Merveille Bope, TP Mazembe walionekana kucheza kwa umakini na uzoefu mkubwa, kitu ambacho kimeisaidia kupata point tatu.
Kwa matokeo hayo Yanga anakuwa kapoteza mchezo wa pili mfululizo, baada ya mchezo wa kwanza kufungwa kwa goli 1-0 na MO Bejaia ya Algeria, kwa sasa msimamo wa Kundi A unaendelea kuongozwa na TP Mazembe wenye point sita wakifuatiwa na MO Bejaia wenye point tatu, lakini wamezidiwa mchezo na TP Mazembe na Yanga.
Angalia hali ilivyokuwa uwanjani asubuhi