Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo Zitto Kabwe jana tarehe 7/6/2016 aliitwa Polisi na Mkuu wa Upelelezi wa Kanda Maalumu ya Dar es salaam ACP Camilius Wambura.
Kwa mujibu wa Katibu Itikadi, Mawasiliano na Uenezi wa chama hicho Ado Shaibu, amesema ACP Wambura amemuita Zitto Kabwe kuhojiwa ikiwa ni siku moja imepita tangu azindue operesheni Linda Demokrasia ambayo inatarajiwa kuzunguka nchi nzima kupinga ukandamizwaji wa Demokrasia nchini
Amesema licha ya Zitto kuitwa na Mkuu wa Upelelezi wa Kanda Maalumu ya Dar es salaam Wambura aliomba Zitto asiende jana kwa kuwa ni karibu na masaa ya kufuturu na kumtaka aende leo saa tatu asubuhi.
Kwa upande mwingine Shaibu amesema Chama cha ACT-Wazalendo kitawasiliana na wanasheria wao ili kupata tafsiri ya kimahakama ya uhalali wa jeshi la polisi kuzuia mikutano ya vyama vya siasa ambayo inatambuliwa na kulindwa na katiba.
Social Plugin