Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

Mdau wa Malunde1 blog ,Mheshimiwa David Nkulila Afunga Ndoa Mjini Shinyanga,Tazama Picha 20 Hapa




Jumapili ya Julai 24,2016 mchana ,mdau wa Malunde1 blog mheshimiwa David Mathew Nkulila amefunga ndoa na bi Prisca Makamba. 



Ibada ya ndoa ya Nkulila aliyekuwa naibu meya wa manispaa ya Shinyanga na sasa ni diwani wa Kata ta Ndembezi katika manispaa ya Shinyanga David Nkulila na Prisca Makamba imefanyika katika kanisa Katoliki la Mama Mwenye Huruma lililopo Ngokolo Mjini Shinyanga. 

Mwandishi wetu Kadama Malunde ametusogezea  picha 20 za harusi ya wapendwa hawa.
Ndani ya kanisa Katoliki la Mama Mwenye Huruma lililopo Ngokolo Mjini Shinyanga.
Kanisani
Ndoa ikiendelea kufungwa
Ndoa ikiendelea kufungwa
Zoezi la kuvalishana pete ya ndoa linaendelea
Nkulila akimvalisha pete ya ndoa bi Prisca
Wanandoa wakionesha pete za ndoa
Zoezi la kusaini vyeti vya ndoa 
Nkulila akisaini cheti cha ndoa
Prisca akisaini cheti cha ndoa
Nkulila na Prisca wakionesha vyeti vyao vya ndoa

Mwenyekiti wa Mtaa wa Dome Solomon Naringa Najulwakatika kata ya Ndembezi bwana na diwani wa kata ya Ngokolo Mheshimiwa Emmanuel Ntobi wakiwa kanisani


Aliyekuwa diwani wa kata ya Ngokolo Sebastian Peter akimpongeza Nkulila kwa kufunga ndoa nje ya kanisa baada ya ibada ya ndoa kumalizika
Pongezi zikaendelea kutolewa
Pongezi zinaendelea kutolewa
Picha ya kumbukumbu
Kulia ni Mkurugenzi wa Malunde1 blog pia mwenyekiti wa klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga bwana Kadama Malunde akipiga selfie na wanandoa hao
Mdau wa Malunde1 blog na rafiki kipenzi wa Mheshimiwa David Nkulila bwana Ommy Fashion akiwa ndani ya gari kwa ajili ya 
kuendelea na msafara wa maharusi hao
Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com