Julai 23,2016 Taasisi ya Brigite Foundation imezindua mradi wa taa za solar katika kituo cha walemavu wa ngozi cha Buhangija katika manispaa ya Shinyanga kwa ajili ya kuimarisha usalama katika kituo hicho ambacho sasa kina jumla ya watoto albino 220,wasiosikia 61 na wasioona 33.
Uzinduzi huo umefanywa na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro ambapo mbali na uzinduzi huo wa mradi wa umeme mbadala,watoto katika kituo hicho walishiriki michezo mbalimbali pamoja na kula chakula cha pamoja na viongozi wa taasisi ya Brigitte Alfred Foundation na kampuni ya wakandarasi umeme ya CSI Electrical Limited inayojihusisha na kutengeneza na kufunga miundo mbinu ya umeme (picha zipo hapo chini).
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi huo,Rais na Mwanzilishi wa Brigitte Alfred Foundation bi Brigitte Alfred alisema mradi huo mkubwa wa kisasa wa taa za sola utasaidia kwa kiasi kikubwa kuimarisha usalama wa watoto hao katika kituo hicho.
Brigitte ambaye ni Miss Tanzania mwaka 2012 alisema baada ya kuguswa na hali iliyopo katika kituo hicho mwaka jana aliomba Kampuni ya Wakandarasi wa Umeme -CSI Electrical Limited kusaidia kufunga umeme katika kituo hicho wakakubali na hatimaye leo mradi huo umezinduliwa.
“Tunaushukuru uongozi wa CSI Electrical Limited kwa namna walivyopokea maombi yetu na hatimaye kuchukua hatua za haraka kwa kutoa msaada huu pia viongozi wa serikali na chama cha watu wenye ulemavu wa ngozi kwa ushirikiano wenu uliosaidia kukamilika kwa mradi huu”,alieleza Alfred.
“Mradi huu umetimiza na kuunga mkono malengo ya Millenia namba 7 inayolenga upatikanaji wa nishati salama “Affordable and clean energy”,tunatarajia mradi huu utahamasisha na kuchochea ari ya wanafunzi katika elimu ya mazingira na matumizi ya nishati mbadala na watawawezesha kusoma na kushiriki kwa vitendo katika kufikia malengo ya kitaifa na ya kidunia kama kizazi na viongozi wa kesho”,aliongeza.
Hata hivyo alitumia fursa hiyo kuiomba jamii kuunga mkono juhudi za serikali na kusimamia kauli mbiu ya pamoja ya kuhimiza amani,upendo na kutokomeza kabisa matukio maovu kwa watu wenye ulemavu wa ngozi na kuifanya Tanzania endelee kuwa mahala pazuri na salama pa kuishi.
Kwa upande wake mwakilishi wa Kampuni ya wakandarasi wa umeme -CSI Electrical Limited, Joan Kahwa alisema wamefunga Panel 26 na mradi huo umegharimu kiasi cha shilingi milioni 75.88.
“CSI ilipokea ombi la taasisi ya Brigitte Alfred Foundation kwa moyo wote ili kuungana nao katika kuboresha maisha ya watoto wetu hapa Buhangija,Mkurugenzi Mtendaji wa CSI Elecrical Limited alitembelea kituo hiki mwaka 2015 ili kutafiti jinsi ya kukisaidia,katika ziara hiyo tuligundua changamoto nyingi zinazowakabili watoto pamoja na walimu na walezi waishio hapa kituoni”,alieleza Kahwa.
“Kwa awamu ya kwanza tuliona ni vyema kuboresha ulinzi wa eneo hili,kwa kudhamini ununuzi,uingizaji,usafirishaji na ufungwaji wa taa za sola shuleni hapa ili kuwe na mwanga wa kutosha nyakati za usiku”,alifafanua.
“Katika awamu ya pili tutalenga kuboresa mfumo wa maji ili upatikanaji wa maji uwe rahisi zaidi kwa kufunga pump ya sola yenye uwezo wa kutosha kwa kituo hiki,jitihada hii itasaidia kuboresha hali ya usafi katika shule hii kwa kurahisisha shughuli za usafi,kufua,kuosha vyombo,kuandaa chakula na usafi wa watoto kwa ujumla”,aliongeza Kahwa.
Naye Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro aliyezindua mradi huo aliipongeza taasisi ya Brigitte Alfred Foundation kwa kushirikiana na kampuni ya wakandarasi wa umeme CSI Electrical Limited kufanikisha kumaliza changamoto ya umeme katika kituo hicho.
Mkuu huyo wa wilaya alitumia fursa hiyo kuwatahadharisha baadhi ya watu wanaowinda watu wenye albinism kwamba serikali haitasita kuwachukulia hatua huku akiwataka wazazi na walezi wa watoto hao kutowatekeleza kituoni watoto hao.
Brigitte Alfred amefanikisha zoezi la kufunga umeme wa solar katika kituo cha Buhangija mwaka mmoja tu baada ya kukamilisha ujenzi wa bweni la kisasa la wanafunzi katika kituo hicho cha Buhangija mwaka 2015 linalowezesha kuishi watoto 70 ambalo lilizinduliwa na kukabidhiwa mwaka 2015.
Mwandishi mkuu wa Malunde1 blog,bwana Kadama Malunde alikuwepo eneo la tukio ametuletea picha 60 za matukio yaliyojiri..Tazama hapa chini
Mafundi umeme kutoka kampuni ya wakandarasi wa umeme CSI Electrical Limited wanaojihusisha na kutengeneza na kufunga miundo mbinu ya umeme wakiendelea na zoezi la kufunga mitambo ya umeme wa solar katika kituo cha watoto wenye ulemavu wa ngozi (albino),wasiosikia na wasioona cha Buhangija katika manispaa ya Shinyanga.Kila mtambo una panel 2 na jumla ya panel zilizofungwa kituoni hapo ni 26.
Mafundi umeme wakiendelea kufunga moja ya mitambo ya umeme unaotumia nguvu ya jua katika kituo cha Buhangija...Kila mtambo una Panel 2 na jumla ya Panel zilizofungwa katika kituo hicho ni panel 13,thamani ya mradi wote ikiwa ni shilingi milioni 75.88
Mgeni rasmi katika uzinduzi wa mradi wa Umeme wa Solar katika kituo cha Buhangija,Josephine Matiro akiwasili katika kituo hicho na kupokelewa na watoto wanaoishi katika kituo hicho
Mwakilishi wa Kampuni ya wakandarasi wa umeme -CSI Electrical Limited Joan Kahwa(katikakti) akimuonesha mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro (kulia) akimuonesha moja ya mitambo ya umeme wa jua katika kituo cha Buhangija.Kushoto ni Miss Tanzania 2012 Brigitte Alfred aliyefanikisha kuwepo kwa mradi huo
Mkuu wa wilaya Josephine Matiro na viongozi mbalimbali wakiangalia mtambo wa umeme wa solar
Mwakilishi wa Kampuni ya wakandarasi wa umeme -CSI Electrical Limited Joan Kahwa akimuongoza mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine kuangalia mitambo ya umeme wa jua katika kituo cha Buhangija
Nyuma ya bweni lililojengwa na Miss Tanzania 2012 ,Brigitte Alfred -Kushoto ni mratibu wa Brigitte Alfred Foundation Stanley Mosha akimueleza mkuu wa wilaya kuhusu faida za mradi huo ambao utasaidia kwa kiasi kikubwa kuimarisha ulinzi na usalama katika kituo hicho
Kushoto ni mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akiangalia mtambo wa umeme wa jua uliopo karibu na bweni lililojengwa na Miss Tanzania 2012 Brigitte Alfred
Mkuu wa wilaya akiendelea kuangalia mazingira ya kituo cha Buhangija
Bweni lililojengwa na Miss Tanzania 2012 Brigitte Alfred
Mgeni rasmi ambaye ni mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akikata utepe ishara ya kuzindua mradi wa umeme wa Solar katika kituo cha Buhangija katika manispaa ya Shinyanga
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akikata utepe.Uzinduzi huo umehudhuriwa na viongozi wa taasisi ya Brigitte Foundation,viongozi wa Chama watu wenye Ulemavu wa ngozi Tanzania (TAS),viongozi wa Kampuni ya wakandarasi wa umeme -CSI Electrical Limited,wakuu wa idara ya elimu makundi maalumu,mkurugenzi wa manispaa ya Shinyanga,walimu na watoto wanaolelewa katika kituo hicho.
Mwalimu mkuu wa shule ya Msingi Buhangija Seleman Kipanya ambaye pia ni msimamizi wa kituo cha watoto wenye ulemavu cha Buhangija akizungumza ambapo alisema kituo hicho sasa kina jumla ya watoto 314
Rais na Mwanzilishi wa Brigitte Alfred Foundation bi Brigitte Alfred akizungumza katika kituo cha Buhangija ambapo alisema mradi huo utakuwa msaada mkubwa kwa maisha ya watoto hao kituoni hapo kwa ajili ya mwanga
Rais na Mwanzilishi wa Brigitte Alfred Foundation bi Brigitte Alfred akitoa hotuba yake ambapo alisema Brigitte ameongeza kuwa mradi huo utasaidia kituo hicho kuwa na umeme wa uhakika kwa gharama nafuu na kuchochea ari ya wanafunzi katika elimu ya mazingira na matumizi ya nishati mbadala.
Rais na Mwanzilishi wa Brigitte Alfred Foundation Brigitte Alfred alisema taasisi yake inatambua uwepo wa vituo vingi vilivyo na mahitaji tofauti mfano kituo cha Kabanga Kasulu mkoani Kigoma hivyo aliwahimiza wadau mbalimbali kuungana pamoja katika kuwasaidia watoto.
“Naomba tuhakikishe kuwa watoto hawa wanarudi kujumuika,kuungana na kushiriki na jamii katika ujenzi wa taifa kwa pamoja,kila mmoja wetu ahakikishe anafanikisha kuwezesha watoto hawa wanajumuishwa katika jamii na siyo vinginevyo,tunaomba vyombo vya habari kusaidia jitihada hizi”,aliongeza Brigitte Alfred.
Miss Tanzania 2012 Brigitte Alfred akitoa hotuba yake
Miss Brigitte akiendelea kutoa hotuba yake
Miss Brigitte akifurahia jambo
Mwakilishi wa Kampuni ya wakandarasi wa umeme -CSI Electrical Limited Joan Kahwa akielezea kuhusu mradi wa umeme wa solar katika kituo cha Buhangija.Alisema lengo la CSI ni kusaidia shughuli za kuendeleza elimu,michezo,kuboresha afya na kutunza mazingira kwa watoto wenye ulemavu mbalimbali wakie wa ngozi na wasioona,wasiosikia na wenye ulemavu mbalimbali,tunaamini ulemavu siyo kikwazo kwa watoto kufikia malengo yao ya kimasomo na kimaisha
Tunafuatilia kinachoendelea hapa...
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akizungumza katika kituo cha Buhangija ambapo mbali na kupongeza jitihada za Miss Tanzania mwaka 2012 kufanikisha kupatikana kwa huduma ya umeme katika kituo hicho aliwaomba wadau wengine kufika katika kituo hicho kwani matatizo ya kituo hicho hayawezi kumalizwa na serikali pekee
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akizungumza
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akisisitiza jambo
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro alitumia fursa hiyo kuwakemea watu wote wanaowinda watu wenye albinism na kuongeza kuwa serikali haitasita kuwachukulia hatua kali wakibainika
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akisisitiza jambo
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akiendelea kuzungumza
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akipanda mti wa kumbukumbu katika kituo cha Buhangija
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro na Rais na Mwanzilishi wa Brigitte Alfred Foundation bi Brigitte Alfred wakipanda mti
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro na Rais na Mwanzilishi wa Brigitte Alfred Foundation bi Brigitte Alfred wakimwagilia maji mti walioupanda
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akisisitiza jambo baada ya kupanda mti
Msimamizi wa Kituo cha Buhangija Seleman Kipanya na mratibu wa Brigitte Alfred Foundation Stanley Mosha wakipanda mti
Watoto wakicheza muziki mbele ya mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro
Mwanzilishi wa Brigitte Alfred Foundation Brigitte Alfred akicheza muziki na watoto
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akifungua michezo kwa watoto,walimu na walezi wa watoto katika kituo cha Buhangija
Tunasubiri kuona michezo ya watoto,walimu na walezi wa watoto..
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akiteta jambo na Rais na Mwanzilishi wa Brigitte Alfred Foundation Brigitte Alfred
Rais na Mwanzilishi wa Brigitte Alfred Foundation Brigitte Alfred akiangalia shindano la kuchora
Kushoto ni mwakilishi wa Kampuni ya wakandarasi wa umeme -CSI Electrical Limited Joan Kahwa,Rais na Mwanzilishi wa Brigitte Alfred Foundation Brigitte Alfred na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro wakishuhudia jinsi watoto wanavyochora vitu mbalimbali
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akachukua kalamu kwa ajili ya kuchora
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro naye akaamua kuanza kuchora
Shindano la mbio za magunia likaendelea
Watoto katika kituo cha Buhangija
Mchezo wa kuvuta kamba ukiendelea kati ya walimu na walezi wa watoto katika kituo cha Buhangija likiendelea
Katika shindano hilo walezi wa watoto (kushoto) waliibuka washindi
Mratibu wa taasisi ya Brigitte Foundation bwana Stanley Mosha akieleza jinsi taasisi yao inavyojali watoto katika maeneo mbalimbali nchini Tanzania ikiwemo kituo cha Kabanga mkoani Kigoma
Rais na Mwanzilishi wa Brigitte Alfred Foundation bi Brigitte Alfred (wa pili kushoto) akifurahia jambo
Mwenyekiti wa ALAT taifa na mstahiki meya wa manispaa ya Shinyanga,mheshimiwa Gulam Hafeez Mukadam akizungumza katika kituo cha Buhangija ambapo aliipongeza taasisi ya Brigitte Alfred Foundation kwa kujali watoto ambapo wamejenga bweni na kufanikisha kufungwa kwa umeme wa solar
Mwenyekiti wa ALAT taifa na mstahiki meya wa manispaa ya Shinyanga,mheshimiwa Gulam Hafeez Mukadam alitumia fursa hiyo kuwaomba wadau mbalimbali kuendelea kuwasaidia watoto hao kwani ni dhawabu kubwa kusaidia watoto hao wenye mahitaji maalum
Mwenyekiti wa ALAT taifa na mstahiki meya wa manispaa ya Shinyanga,mheshimiwa Gulam Hafeez Mukadam aliyekuwa ameambatana na mwenyekiti wa wapanda baiskeli Shinyanga bwana Tungu Johnson (wa pili kushoto) aliwapongeza pia Waendesha baiskeli katika manispaa ya Shinyanga kuona umuhimu wa kutoa msaada wa chakula ikiwemo maharage kilo 40,mchele kilo 80,unga wa sembe kilo 85,mafuta ya kupikia lita 10 na tenga la nyanya vyote vikiwa na thamani ya shilingi 300,000/- kwa ajili ya watoto hao
Muda wa chakula ukawadia- Watoto wakiwa katika foleni kwa ajili ya chakula kilichoandaliwa na taasisi ya Brigitte Alfred Foundation na CSI Electrical Limited (picha zipo hapo chini).
Chakula na vinywaji vikiwa tayari kwa ajili ya watoto wenye albinism,wasioona na wasiosikia katika kituo cha Buhangija katika manispaa ya Shinyanga
Watoto wakichukua chakula
Watoto wakiendelea kula chakula
Watoto wenye ulemavu wa kutoona wakichukua chakula
Miss Tanzania 2012 Brigitte Alfred akimlisha chakula mmoja wa watoto katika kituo cha Buhangija katika manispaa ya Shinyanga
Zoezi la kula likiendelea
Kushoto ni mwakilishi wa Kampuni ya wakandarasi wa umeme -CSI Electrical Limited Joan Kahwa akimpa soda mtoto mwenye albinism katika kituo cha Buhangija katika manispaa ya Shinyanga.
Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog