Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

Askari Polisi Auawa Kwa Kupigwa Risasi Akiongoza Magari Barabarani Jijini Dar es Salaam


Askari wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Sajenti Mensah wa Kituo cha Polisi Oysterbay ameuawa usiku wa kuamkia leo kwa kupigwa risasi akiwa kazini eneo la Sayansi Kijitonyama jijini Dar es Salaam.



Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Christopher Fuime amesema tukio hilo lilitokea jana majira ya saa mbili usiku  na chanzo cha mauaji hayo hakijafahamika. 



“Tukipata chanzo itakuwa tayari upelelezi wetu umetimia, hivyo kwa sasa tunalifanyia kazi ili kubaini wahusika wa mauaji hayo,” amesema Fuime.
 Chanzo-Mpekuzihuru.com
 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com