Tamko
la Chadema limetolewa na Katibu Mkuu wa chama hicho Kanda ya Ziwa
Magharibi, Meshack Micus alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari
jana ofisini kwake.
“Sisi
kama Chadema kanda ya Ziwa hasa kanda ya Victoria tayari
tumeshawaelekeza wanachama wetu wote, viongozi wetu wote na tayari
mwitikio ni mzuri. Na hadi leo tayari viongozi wetu wa vitongoji 1973
wameshajiandaa wako tayari kwa ajili ya kufanya maandamano na kufanya
mikutano ya hadhara katika maeneo yao,” alisema.
“Tutaandaa
maandamano kutokea Kyelwa, tutaelekea Misenyo, Bukoba vijijini na
tutakuja moja kwa moja mpaka Chato. Na wa Mwanza tayari nimeshawaagiza
kwamba maandamano yetu tunaenda kuyafungia Chato,” aliongeza.
Tamko
hilo limekuja ikiwa ni siku moja baada ya Rais John Magufuli kuwaonya
Chadema kutomjaribu kwa kufanya maandamano bila kufuata utaratibu kwani
hatawavumilia.
Rais
Magufuli aliwataka wananchi kutokubali kudanganyika na kufanya
maandamano na badala yake wajikite katika kufanya kazi itakayowaletea
maendeleo.
Mwenyekiti
wa Chadema, Freeman Mbowe alitangaza kile walichokiita ‘Umoja wa
Kupambana na Udikteta Tanzania (UKUTA)’, akiwaalika wafuasi wake kufanya
maandamano nchi nzima kuanzia Septemba Mosi mwaka huu.