Akizungumza na vijana hao jana jijini Dar es salaam Mashinji aliwaambia
vijana hao chama chao kimejipanga kushika dola hivyo wao kama vijana
wanatakiwa kuhakikisha wanatekeleza majukumu ya kufanya uchaguzi na
kuwatambua wanachama hai, pia kuhakikisha kuwa uchaguzi wa serikali za
mitaa vijana wanashiriki nafasi mbali mbali na kushinda
”Nataka
niwape majukumu matatu ambayo mkiyafanya hayo 2020 tutashinda
nakutangazwa, moja hakikisheni tunaingiza wanachama wapya na kuwahakiki
walio hai, nendeni 2019 kwenye serikali za mitaa vijana mgombee na
tupate viongozi ngazi ya chini viijana wasomi, na tatu kwa mwaka huu
kila kijana ajue nafasi zitakozogombewa katika eneo lake hiyo
itatusaidia kushinda nafasi nyingi za madiwani kwa Tanzania bara na
visiwani na haya ndiyo majukumu makubwa ninayowapatia” Alisema Mashinji.
Pamoja na hayo aliwataka
vijana hao kuendelea kupigania haki za wanyonge na kushinda vita ya
demokrasia bila kuvunja sheria huku akiwaasa kuwa askari mzuri na shujaa
ni yule anayepambana bila risasi.
”Askari
mzuri ni yule ashindaye vita bila kutumia risasi zake, mkawe mabalozi
wa kuwatetea wanyonge na haki zao, msiwe waoga kudai katiba ya wananchi,
pia kuna watu Geita, Shinyanga na Simiyu tunataarifa wanapigwa kisa
itikadi ya upinzani wa vyama hivyo kama vijana mnatakiwa mpaze sauti kwa
ajili yao”. aliwaambia Mashinji.
Hata hivyo Mashinji aliwaasa vijana hao kuwa wapole na kusubiri maamuzi ya viongozi wa chama kwani yanabusara. Aidha aliwapongeza vijana hao kwa kuwa na umoja wa kupigania haki na misingi ya demokrasia.
Mwenyekiti wa Bavicha Taifa Patrobas Katambi alimweleza
Katibu huyo wa chama kuwa wao wapo tayari kwa pambano japo wanasikiliza
na kutii kauli ya chama hivyo wao watatoa msimamo wao.
”Sisi
vijana tupo tayari miili yetu ilale makaburini na tukumbukwe kama
mashujaa waliokufa wakipigania haki, tumesikiliza maagizo ya viongozi
wetu lakini pia sisi leo tutatoa msimamo wetu”.- Katambi
Social Plugin