Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

Chama Cha Soka Cha England FA Kimemtangaza Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa



Ijumaa ya Julai 22 2016 chama cha soka cha England FA kimemtangaza kocha wa klabu ya Sunderland ya England Sam Allardyce “Big Sam” kuwa kocha mkuu wa timu ya taifa ya England. FA wametangaza leo rasmi na kukamilisha ule uvumi wa muda mrefu kuhusiana na kocha huyo kuchukua nafasi hiyo.

Sam Allardyce mwenye umri wa miaka 61 anaingia kuifundisha timu ya taifa ya England kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na Roy Hogson, Big Sam amesaini mkataba wa miaka miwili wa kuifundisha England, ambapo ataiongoza timu hiyo hadi katika fainali za Kombe la dunia 2018 Urusi.



Kama utakuwa unakumbuka vizuri Sam Allardyce ambapo wengine wanapenda kumuita “Big Sam” amewahi kuvifundisha vilabu vya Bolton, Newcastle, Blackburn, West Ham na Sunderland na sasa ameingia kuifundisha timu ya taifa ya England.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com