Alinusurika
kuuawa baada ya majambazi hao waliokuwa na bunduki na bastola
kumfyatulia risasi sita alipokuwa akiwafukuza ambazo hata hivyo,
hazikumpata.
Tukio
hilo ambalo lilionekana kama sinema, lilitokea mwishoni mwa wiki baada
ya majambazi hao kuvamia duka la jumla la kuuza mitumba linalomilikiwa
na Menti Mbowe na kupora Sh10 milioni.
Katika
tukio hilo lililotokea saa tano asubuhi eneo la Kiborlon, majambazi hao
walimjeruhi kichwani mfanyabiashara huyo anayemiliki pia mabasi ya
Machame Safaris.
Hali
ya majeruhi huyo inaendelea vizuri. Akisimulia tukio hilo, diwani huyo
alisema siku hiyo akiwa maeneo ya Kiborlon, alipigiwa simu kuwa
mfanyabiashara huyo amevamiwa na majambazi ndipo alipoendesha gari lake
hadi eneo la tukio.
“Nilipofika
pale wale majambazi watatu ndiyo walikuwa wanatoka kwenye duka.
Nikampelekea gari yule aliyekuwa ameshika bunduki. Kuona hivyo akafyatua
risasi hewani,” alisema Kagoma.
“Yule
mwenye bunduki akaingia uchochoroni kuelekea Barabara ya Stendi ya
Kidia. Mwenzake aliyekuwa na bastola naye akawasha risasi nyingine
hewani kunitisha,” alisema.
Baada
ya hali hiyo, diwani huyo alilazimika kujificha kwenye gari na
majambazi hao walidandia pikipiki na kuanza kukimbia kuelekea Barabara
ya Msaranga, naye akawafuata kuelekea huko.
“Wakati
huo tayari vijana wangu wa bodaboda wakawa nao wamesikia hilo tukio
tukaanza kusaidiana kuwafukuza lakini mbele kidogo pale Msaranga wale
majambazi wakasimamisha pikipiki yao umbali wa mita 30 kutoka nilipokuwa
na mmoja wao mwenye bunduki alifyatua risasi mbili na mwenye bastola
risasi mbili kuelekea uelekeo wangu.
“Nililazimika
kujificha kwenye kiti, wale majambazi wakajua wameniua. Wakapanda tena
pikipiki ili watoroke. Nikawasha tena gari huku vijana wangu nao
wakinisaidia tukaanza kuwafukuza,” alisema.
Kagoma
alisema majambazi hao walipita maeneo ambayo gari haliwezi kupita
wakaelekea eneo la Mabogini Moshi Vijijini hadi lango la TPC na baadaye
wakaelekea Rundugai wilayani Hai.
“Kuna
eneo vijana wangu wanasema kulikuwa na vumbi sana, ndipo walipowapoteza
na majambazi wakatoroka kupitia njia ya reli ili kukwepa polisi
waliokuwa wakiwasubiri mbele,” alisema na kuongeza: “Hatukuwa na
silaha, lakini tulijitahidi kupambana nao kwa ujasiri. Tatizo nafikiri
tulikosea kidogo. Ilitakiwa wakati tukifukuzana nao tuwape polisi
uelekeo wa majambazi.”
Kamanda
wa Polisi Mkoa Kilimanjaro, Wilbroad Mutafungwa alisema jana kuwa Jeshi
lake litatoa taarifa rasmi kwa wanahabari leo kuhusiana na msako
unaoendeshwa na jeshi hilo.
“Kuna
mambo tumeyafanya tangu tukio hilo litokee lakini kesho (leo) saa sita
mchana tutatoa taarifa rasmi pamoja na mafanikio tuliyofikia hadi sasa.
Tunaendelea vizuri na upelelezi,” alisema.
Kamanda
Mutafungwa, alitoa wito kwa wananchi kutoa ushirikiano kwa jeshi hilo
ikiwamo kuwafichua wahalifu na mbinu wanazozitua akisema polisi
wamejipanga kukabili wimbi jipya la ujambazi.
Social Plugin