Jinsi Ureno Ilivyofuta Uteja wa Miaka 40 Dhidi ya Ufaransa Kwa Kutwaa Kombe la Euro 2016

 
Usiku wa Julai 10 2016 wapenda soka duniani kote macho na masikio yao yalikuwa Paris Ufaransa kushuhudia fainali ya 51 ya michuano ya Euro, Paris ulichezwa mchezo wa fainali ya Euro 2016 kati ya timu ya taifa ya Ureno dhidi ya mwenyeji Ufaransa ambaye mara ya mwisho kufungwa na Ureno ilikuwa April 26 1975.

Huu ni mchezo ambao ulikuwa unachezwa lakini nafasi kubwa ya ushindi ilikuwa inapewa Ufaransa kutokana na rekodi yake ya miaka 40 kutofungwa na Ureno, lakini pamoja na uwezo wao waliouonesha katika michuano ya Euro mwaka huu, Ureno matumaini yalipotea zaidi dakika ya 23 baada ya nahodha wao Cristiano Ronaldo kushindwa kuendelea na mchezo kwa kuumia.



Mchezo ulikuwa mgumu licha ya Ufaransa kuongoza kwa kumiliki mpira kwa asilimia 54 kwa 46, dakika 90 zilimalizika kwa suluhu, hivyo refa akaongeza dakika 30 zilioenda kuimaliza Ufarasa, Ureno walifanikiwa kuibuka a ushindi wa goli 1-0, goli pekee ambalo lilifungwa na Eder Antonio dakika ya 109, Eder aliingia akitokea benchi dakika ya 79.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post