Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

Kikwete Ampa Tahadhari Rais Magufuli Kuhusu CCM na Wana CCM,Asema Uenyekiti Siyo Lelemama


JAKAYA Kikwete, Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) anayemaliza muda wake amemtahadharisha mwenyekiti mtarajiwa wa Chama hicho John Magufuli kwa kumweleza kuwa uenyekiti ndani ya CCM siyo lelemama kwani wajumbe wasipoelewa wanachokitaka.



Mbali na kumpa tahadhari hiyo pia alikiri kuwa mwaka jana chama hicho kilikumbwa na misukosuko mingi ambayo ingeweza kukifanya chama hicho kuanguka kwani kilikuwa na mafisi wengi ambao walikuwa wakisubiri mkono udondoke ili washibe


Ametoa kauli hiyo leo wakati wa ufunguzi wa mkutano wa Halmashauri Kuu ya chama hicho ambayo ajenda ilikuwa moja tu ya kujadili na kupitisha jina la mwenyekiti ambalo litapelekwa katika mkutano mkuu kwa lengo la kupigiwa kura.


Kikwete amesema ..."CCM ilikuwa ivunjike wakati wa kipindi kigumu cha uchaguzi wa mwaka jana lakini tunamshukuru Mungu kwa kuwa tumeweza kukaa imara na kukitafa chama kutovunjika.


“Tunasema kikao kama hiki hatumwi mtoto tunakuja wenyewe kikao cha leo ni kikao cha kihistoria, kwa mamna mbili kwanza ni kikao changu cha mwisho, nikija kwenye NEC ni pale mtakapo nialika lakini tulikubaliana kwamba wazee hao wameishatumikia vya kutosha na tuwaache wapumzike utaratibu wa hapo nyuma ukimaliza uenyekiti unakuwa mjumbe wa kudumu wa kamati kuu na halmashauri kuu.


“Siku moja Mzee Mkapa akasema bwana mbona sisi wazee mnatusumbua sana mnatuita kila siku na sisi tumeishakuwa wazee tunakaa mpaka saa saba usiku kwa hivi sasa tuacheni, ndipo niliposema hatuwezi na tukaamua kuunda baraza la wazee.


“Tukaona hatuwezi kuwaita kila siku lakini tunawatengenezea baraza la wazee ambalo ni baraza la ushauri kimsingi linahitajika kwa jambo muhimu sana kama ilivyo kuwa mwaka lakini nilijadiliwa nikaambiwa JK hataki wazee lakini nikasema huo ni uamuzi wa busara kabisa” amesema Kikwete.


“Kuna maswala makubwa ya chama chetu na uhai wake kama ilivyokuwa mwaka wa jana, eeee chama chetu kilikuwa kimekaa katika msukosuko mkubwa mnaingia hapa watu wanaimba hiki wanaimba kile mjadala mkali lakini nikasema tutavuka tu maadamu tupo ndiyo changamoto ya uongozi.


“Na maadamu CCM haikuvunjika mwaka wa jana haitavunjika tena, maana mafisi yalikaa hapa yanasubiri mkono udondoke lakini haukudondoka na maadam haukudondoka mwaka wa jana CCM haidondoki,”amesema Kikwete.


Amesema rais atakuwa mwenyekiti na wakati mwingine kuna wakati kikao kinakuwa kigumu kwani wajumbe wanataka kutendewa haki wa wasipopata haki zao wanakuwa wakali sana.


Amesema halmashauri kuu ni kikao Muhimu cha uongozi pale ambapo hakuna mikutano ya chama amesema kamati kuu ni kikao cha kusimamia shughuli muhimu za chama na NEC ni kikao cha juu cha kutoa viongozi.


Amesema wajumbe wa vikao ni wepesi sana kusifia lakini wanakuwa wakali sana pale ambapo mambo yanaenda vibaya hivyo kiongozi ni lazima kumsikiliza na kujua nini ambacho wajumbe wanataka.


Amesema wajumbe hao wanakuwa wakali kwa kuwa wanataka mambo ndani ya chama yaende vizuri ili nao ndani ya chama waweze kujivunia.


Mbali na hayo amesema wajumbe wanatakiwa kushirikiana na mwenyekiti mpya ili kukifanya chama kuweza kusonga mbele zaidi.





Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com