Maafisa wa TAKUKURU Wakamatwa Wakipokea Rushwa Huko Njombe



 Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoa wa  Njombe  inawashikilia watumishi wake wawili wa wilaya ya Makete  kwa tuhuma za kuomba rushwa  ya shilingi laki sita kwa mwananchi   jina lake  limehifadhiwa  kwa usalama wake ambaye alikuwa anakabiliwa na tuhuma za kugushi vyeti  vya ajira  wilayani humo.


Kamanda wa TAKUKURU mkoa wa Njombe Charles Nakembetwa amewataja watuhumiwa hao kuwa ni pamoja na  mwanasheria wa taasisi ya TAKUKURU wilaya ya Makete Frednand  Nsakuzi pamoja na mlinzi  wa ofisi ya TAKUKURU Makete Julius  Hassan  wote watumishi wa taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa wilani Makete.


Amesema watuhumiwa hao kwa pamoja  waliomba kiasi hicho cha fedha shilingi laki sita kwa  mwananchi ambaye jina lake limehifadhiwa  June 28  mwaka huu majira ya  saa moja na saa mbili usiku  ambapo waliomba rushwa  kwa  mwananchi huyo aliyekuwa anatuhumiwa kugushi vyeti vya ajira.


Nakembetwa amesema watuhumiwa hao  walifanikiwa kupokea fedha ya awali shilingi laki moja   ambapo  baada ya TAKUKURU mkoa wa Njombe kupata taarifa hizo walifanikiwa kuweka mtego ulio wanasa watuhumiwa hao.

Amesema walifanikiwa  kuwakamata  wahusika wakiwa  wanachukua fedha hizo kinyume na kifungu cha  15 cha sheria  ya kuzuia na kupambana na rushwa namba 11  ya mwaka 2007.

Mercy  James-Malunde1 blog Njombe

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post