MKUU
wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, amesema tangu alipotangaza
kuanza kukamatwa kwa mashoga, amebaini kuna mkakati unawaohusisha watu
hao zaidi ya 150 kutaka kumwangamiza.
Kauli
hiyo aliitoa jana Dar es Salaam baada ya kumaliza mahojiano katika
kituo cha redio Clouds FM, ambako alikuwa akifafanua hoja na changamoto
mbalimbali za mkoa wake.
Alisema kuwa baada ya kubainika kwa mipango hiyo, mashoga wanane wamekamatwa na Jeshi la Polisi kwa hatua zaidi.
“Lazima
watu wajue jitihada na harakati za kusimamia katiba na usawa hapa
nchini. Hakuna anayezipenda, vita inakuwa kubwa… Nimebaini kuwa mashoga
zaidi ya 150 waliketi katika baa moja Kinondoni wakipanga njama za
kunimaliza kwa namna moja ama nyingine, lakini kutokana na taarifa za
kiintelijensia, watu kadhaa, wengi wao wakiwa ni mashoga
wameshakamatwa,” alisema Makonda.
Katika
hatua nyingine, Makonda aliwatolea uvivu watu wanaosambaza ujumbe wa
tofauti juu ya maagizo yake katika mitandao ya kijamii, ikiwamo
kutengeneza akaunti feki.
“Kwanza
wanapaswa kujua kuwa sina akaunti ambayo inaanza na cheo changu, hivyo
akaunti zote zangu zimeandikwa kwa jina langu Paul Makonda si
vinginevyo, hivyo kila mtu anapaswa kuwa makini na hilo,” alisema Makonda.
Aliweka
wazi kuwa kuna agizo batili lililowekwa katika mitandao ya kijamii,
akidaiwa kusema kuwa watu wasiokuwa na kazi watakwenda jela, lakini
ukweli ni kwamba ameagiza wenyeviti wa Serikali za mtaa kuhakikisha kuwa
wanafanya uhakiki wa wakazi wao nyumba kwa nyumba kwa ajili ya usalama
wa maeneo wanayoishi.
Aidha
Makonda alisisitiza kuwa kutokana na matatizo yaliyopo, kamwe Hatoacha
kupambana na mafisadi katika halmashauri zote tatu za mkoa wake, pamoja
na wauza unga, wafanyabiashara wa shisha na mashoga.
Social Plugin