NACTE Yatangaza Majina ya Waombaji Udahili Waliochaguliwa Kujiunga Na Kozi Za Cheti Na Diploma

Baraza linapenda kutoa taarifa kuwa Mfumo wa Udahili wa Pamoja (CAS) umefunguliwa tena kuanzia tarehe 22 Julai 2016 ili kujaza nafasi za udahili zilizo wazi baada ya Baraza kuchagua waombaji udahili waliowasilisha maombi yao kuanzia tarehe 4 Machi 2016 hadi tarehe 3 Juni 2016. 
Mwisho wa kuwasilisha maombi ni  tarehe 5 Agosti 2016 saa sita usiku.

Waombaji wapya na baadhi ya waombaji walioshindwa kukamilisha maombi yao kupitia mtandao ilipofika tarehe 3 Juni 2016, wanaarifiwa kuanza kuwasilisha maombi ya udahili kupitia Mfumo wa Udahili wa Pamoja (CAS) ili kujaza nafasi zilizo wazi. Waombaji wanahimizwa kutumia muda huu wa nyongeza ili kuwasilisha maombi.

Baraza linapenda pia kuwaarifu waombaji udahili na umma kwa ujumla kuwa vikao vya Kamati za kuidhinisha majina ya waombaji udahili kupitia Mfumo wa Udahili wa Pamoja (CAS) vilipitisha orodha ya majina  ya wenye sifa za udahili kulingana na nafasi za udahili kwa kila kozi zitolewazo na vyuo husika kati ya tarehe 18 Julai 2016 na 21 Julai 2016. 

Majina ya waombaji waliochaguliwa kwa kila kozi itolewayo na chuo husika yamekabidhiwa vyuoni kupitia Mfumo wa Udahili wa Pamoja (CAS). 

Waombaji waliochaguliwa nao wamearifiwa kupitia kurasa (profile) zao binafsi au kwa kubofya hapa. Waombaji ambao hawakuchaguliwa wamejulishwa sababu zilizowafanya wasichaguliwe kupitia kurasa (profile) zao pia.  

Kwa waombaji wa Shahada ya Kwanza waliowasilisha maombi yao kupitia NACTE, Baraza linapenda kuwaarifu kuwa, mashauriano kati ya NACTE na Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) yanaendelea kufanyika ili kufanikisha udahili wa waombaji wa kozi za Shahada ya Kwanza kama Serikali ilivyoagiza.

Imetolewa na
Ofisi ya Katibu Mtendaji
NACTE
Tarehe: 22 Julai, 2016

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post