Mamia ya wakazi wa mtaa wa Dome kata ya Ndembezi katika manispaa ya Shinyanga na maeneo ya jirani wamejitokeza kwa wingi kuuaga mwili wa kijana mwendesha bodaboda Geofrey Deocres Kazinduki (24) aliyeuawa kwa kuchomwa visu mara tatu tumboni na kifuani na watu wasiojulikana kisha kumpora pikipiki yake.
Kijana Geofrey aliuawa juzi Julai Mosi saa mbili usiku katika barabara ya Shy Bush karibu na relini kata ya Maganzo wilayani Kishapu baada ya mtu asiyejulikana kumkodi kutoka katika stendi ya mabasi yaendayo wilayani mjini Shinyanga.
Inaelezwa kuwa mwendesha bodaboda huyo aliuawa na watu wasiojulikana ambao baada ya kutekeleza mauaji hayo waliondoka na pikipiki yake.
Mwili wa marehemu umeagwa leo na wakazi wa Shinyanga wakiwemo waendesha bodaboda na kesho Julai 04,2016 mwili huo utasafirishwa kwenda nyumbani kwao kijiji cha Nyakibimbili kata ya Katerelo halmashauri ya wilaya ya Bukoba Vijijini mkoani Kagera.
Marehemu ameacha mjane na mtoto mmoja.
Ibada ya kuaga mwili wa marehemu imeongozwa na mchungaji Isaack Masimango kutoka kanisa la KKKT mjini Shinyanga.
Ibada hiyo pia imehudhuriwa na diwani wa kata ya Ndembezi bwana David Nkulila
Mwandishi wa Malunde1 blog,bwana Kadama Malunde alikuwepo msibani ametuletea picha ...Tazama hapa chini
Geofrey enzi za uhai wake akiwa na bodaboda yake |
Jeneza lililobeba mwili wa marehemu likiwa nyumbani kwa marehemu katika mtaa wa Dome kata ya Ndembezi katika manispaa ya Shinyanga
Mchungaji Isaack Masimango kutoka kanisa la KKKT mjini Shinyanga akiongoza ibada ya kuaga mwili wa marehemu Geofrey
Picha ya marehemu Geofrey
Picha ya marehemu ikiwa kwenye jeneza
Waombolezaji
Mchungaji Masimango akiombea mwili wa marehemu
Waombolezaji
Akina mama wakiaga mwili wa marehemu
Zoezi la kuaga mwili wa marehemu likiendelea
Waombolezaji wakiwa nyumbani kwa marehemu
Waombolezaji
Zoezi la kuaga mwili linaendelea
Zoezi la kuaga mwili linaendelea
Zoezi la kuaga mwili wa marehemu linaendelea
Mwenyekiti wa mtaa wa Dome Solomon Naringa Najulwa akiaga mwili wa marehemu,nyuma yake ni diwani wa kata ya Ndembezi David Nkulila
Mwenyekiti wa mtaa wa Dome Solomon Naringa Najulwa akiaga mwili wa marehemu.
Mwenyekiti wa mtaa wa Dome Solomon Naringa Najulwa akiaga mwili wa marehemu,nyuma yake ni diwani wa kata ya Ndembezi David Nkulila
Diwani wa kata ya Ndembezi David Nkulila akiaga mwili wa marehemu
Wana mtaa wakiaga mwili wa marehemu
Zoezi la kuaga mwili linaendelea.
Dr.Ellyson Maeja akiaga mwili wa marehemu
Geofrey Tibakyenda akiaga mwili wa marehemu
Zoezi la kuaga mwili wa marehemu linaendelea
Mkurugenzi wa Malunde1 blog,bwana Kadama Malunde akiaga mwili wa marehemu
Ndugu wakisaidia mke wa marehemu wakati wa kuaga mwili wa mme wake
Ndugu wa marehemu wakiaga mwili wa marehemu
Mchungaji Dr. Meshaki Kulwa kutoka kanisa la AICT Kambarage mjini Shinyanga akiomba wakati wa ibada hiyo
Viongozi wa chama cha waendesha bodaboda katika katika manispaa ya Shinyanga wakiwa msibani
Ndugu wakimtuliza mke wa marehemu
Waandishi wa habari wakiwa msibani
Mwenyekiti wa mtaa wa Dome Solomon Naringa Najulwa akizungumza msibani ambapo alikemea mauaji hayo na kuwataka waendesha bodaboda kuwa makini kwani kuna baadhi yao siyo waaminifu
Waombolezaji
Mwenyekiti wa waendesha bodaboda Jacob Paul akizungumza msibani ambapo aliwataka waenesha bodaboda kuepuka kubeba wateja kwenda nje ya mji kuanzia saa moja usiku
Kushoto ni diwani wa kata ya Ndembezi akizungumza msibani ambapo alisema vitendo vya kihalifu vinasimamiwa na matajiri kwani haiwezekani mtu maskini apore pikipiki,hivyo wanaofadhili uhalifu ni matajiri wenye uhakika wa soko la pikipiki
Nkulila akisisitiza waendesha bodaboda kuwa makini na kulindana
Nkulila akisisitiza jambo
Katikati ni mke wa marehemu
Kushoto ni mjomba wa marehemu bwana Deocres Kamara akizungumza kwa niaba ya familia
Jeneza la marehemu likiingizwa ndani kwa ajili ya safari Julai 04,2016 saa 10 alfajiri
Jeneza likiingizwa ndani ya nyumba ya marehemu
Geofrey enzi za uhai wake |
Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog