BARAZA
la Vijana wa Chadema (Bavicha) limepanga kufanya mkutano wa Kamati ya
Utendaji ya baraza hilo Julai 20, mwaka huu mkoani Dodoma ambao utatoa
mwelekeo wa kupigania demokrasia.
Aidha,
limewataka vijana wa chama hicho nchi nzima kuwa watulivu na kutii
agizo la Mwenyekiti wa chama hicho taifa, Freeman Mbowe wakati
wakisubiri maamuzi ya kikao hicho.
Akizungumza
na waandishi wa habari jana Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Bavicha Taifa,
Patrobas Katambi alisema, baraza hilo linaona kama jeshi la polisi
halitendi haki kwa kuruhusu mkutano wa CCM, jambo alilosema ni
ukandamizaji wa demokrasia.
“Kikao
chetu cha Kamati ya Utendaji tulikuwa tumekiahirisha baada ya polisi
kuzuia, lakini sasa tunafanya tena kwa tarehe ileile ambayo ni Julai 20
mjini Dodoma ambapo tulipanga kufanya mwanzo,” alisema.
Aidha,
Katambi alisema Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Ernest Mangu hana budi
kujiuzulu iwapo mkutano huo wa CCM utafanyika kwa kuwa atakuwa
ameshindwa kusimamia kauli ya jeshi hilo lakini pia ya Rais John
Magufuli.
Alisema
baada ya Mbowe kuwazuia wasiende Dodoma wameamua kuja na mpango wa pili
ambapo hawatakwenda Dodoma lakini hawataruhusu mkutano wa CCM ufanyike
hadi serikali itakapotoa kauli ya haki sawa za kidemokrasia kwa kila
chama.
Katibu
Mkuu wa baraza hilo, Julius Mwita alisema, hawaoni kama kufanyika kwa
mkutano wa kamati ya utendaji kutaathiri kwa namna yoyote usalama wa
wanachama au mkutano wa CCM.
Alisema
tayari hata IGP anajua kuwa watafanya mkutano wao mjini Dodoma lakini
watampa taarifa ukumbi utakaofanyika mkutano huo baada ya kuupata na
kukubaliana na mwenye ukumbi.
Social Plugin