Wanafunzi
waliosimamishwa masomo walikuwa wamegawanyika katika makundi makuu
mawili. Kundi la kwanza lilikuwa ni wanafunzi 6,595 waliodahiliwa katika
Stashahada Maalumu ya Ualimu wa Elimu ya Sekondari na kundi la pili
lilikuwa na wanafunzi 1,210 waliodahiliwa katika mafunzo ya Stashahada
ya Ualimu wa Elimu ya Msingi.
Taarifa iliyotolewa leo na waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Joyce Ndalichako amesema
kwamba baada ya hatua ya kuwaondoa wanafunzi chuoni kuchukuliwa,
Serikali ilifanya Uchambuzi wa wanafunzi hao kwa lengo la kujiridhisha na
sifa zao. Baada ya uchambuzi huo leo Julai 19, 2016 Serikali imetangaza
maamuzi haya…….
Kundi la Stashahada Maalumu ya Ualimu wa Elimu ya Sekondari
Serikali
imesema kwa kuwa uchambuzi umebainisha kuwa Wanafunzi wenye ufaulu wa
Daraja la I na la II ambao pia wamefaulu masomo mawili ya Sayansi kwa
kiwango cha C-A ni 382 (mwaka wa I -134 na mwaka wa II – 248), wanafunzi
hao ndiyo pekee watakaorudishwa katika Chuo Kikuu cha Dodoma ili
wakamalizie mafunzo yao katika Chuo hicho.
Wanafunzi
4,586 wa mwaka wa I wa Programu Maalum ya Stashahada ya Ualimu wa Elimu
ya Sekondari waliokidhi vigezo vya ufaulu watahamishiwa katika Vyuo vya
Ualimu vya Morogoro, Butimba, Mpwapwa, Songea na Tukuyu kuendelea na
masomo yao.
Wanafunzi 1,337 wa Mwaka II watahamishiwa kwenye Vyuo vya Ualimu vya Korogwe na Kasulu kumalizia masomo yao.
Wanafunzi
290 waliokuwa wamedahiliwa kusoma Programu Maalum ya Stashahada ya
Ualimu wa Elimu ya Sekondari Masomo ya Sayansi na Hisabati ambao hawana
sifa stahiki wanashauriwa kuomba mafunzo yanayolingana na sifa walizo
nazo kwenye chuo chochote wanachotaka wao.
Kundi la Programu ya Ualimu wa Elimu ya Msingi
Serikali imesema wanafunzi katika kundi
hili hawakuwa sehemu ya program maalum ya kupunguza uhaba wa walimu wa
Sekondari wa Sayansi na Hisabati. Walikuwa wanaandaliwa kufundisha shule
za msingi wakati lengo la Programu Maalum ilikuwa ni kukabiliana na
tatizo za uhaba wa walimu wa Sekondari. Maudhui ya program waliyokuwa
wanasoma hayakuwa sawasawa na yale ya Programu ya Ualimu wa Sekondari wa
Sayansi na Hisabati.
Wanafunzi
29 wa mwaka wa II wenye Cheti cha Daraja IIIA waliodahiliwa kusoma
Stashahada ya Ualimu wa Shule za Msingi watahamishiwa katika Chuo cha
Ualimu Kasulu wamalizie masomo yao kwa gharama zao wenyewe.
Wanafunzi
1,181 waliodahiliwa kusoma Stashahada ya Kawaida ya Ualimu wa Elimu ya
Msingi waombe mafunzo yanayolingana na sifa walizonazo mahali popote
watakapotaka wao.
Aidha Serikali
imesema itaendelea kuwapatia mikopo wanafunzi watakaorejeshwa UDOM na
wanafunzi watakaohamishiwa kwenye Vyuo vya Ualimu vya Serikali watapewa
mkopo wa kiasi cha Sh. 600,000/= kwa mwaka ambayo ni ada ya Mafunzo ya
Ualimu itakayolipwa moja kwa moja Chuoni.
Social Plugin