NAIBU Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kingwangalla ameagiza Jeshi la Polisi jijini Dar es Salaam kumkamata tabibu maarufu Juma Mwaka ndani ya saa 24
Dk. Kigwangalla ametoa amri hiyo leo jijini Dar es Salaam alipokitembelea tena kituo cha Fore Plan kinachomilikiwa na tabibu huyo maarufu kwa jina la ‘Dk. Mwaka.’
Serikali ilitangaza kukifungia kituo hicho cha afya na vingine vitatu mwezi mmoja uliopita kwasababu zilizoelezwa kuwa ni kutoa huduma kinyume na sheria ambapo kituo cha tabibu Mwaka kilidaiwa kufungiwa kwa mmiliki kujiita daktari badala ya tabibu!
Hata hivyo wiki moja baada ya kuifungia kliniki hiyo kutoa huduma zake, iliendelea kujitangaza kuwa inaendelea kufanya kazi kama kampuni ya ushauri na huduma za kiafya na siyo kliniki tena.
Kutoka jina la awali Fore Plan Clinic ilianza kujitangaza kama Fore Plan Company kitendo ambacho Dk. Kingwangalla amekitaja kuwa ni kinyume na sheria na kuagiza tabibu huyo akamatwe haraka iwezekanavyo.
Social Plugin