Mambo mengi yanatokea duniani ambayo yanaweza yakakushangaza, kusikitisha na mengine yakufurahisha lakini leo Agosti 22, 2016 raia wa India miaka 42 ametolewa visu 40 ndani ya tumbo lake baada ya opersheni aliyofanyiwa hospitali ya Northern Indian city of Amritsari Punjab India iliyofanyika ili kuokoa maisha yake.
Daktari Malhotra aliyeshiriki kumfanyia upasuaji mgonjwa huyo ameripoti CNN na kusema hakuwahi kukutana na kitu kama hicho tangu aanze udaktari na kutaja kuwa mgonjwa huyo amekuwa akimeza visu hivyo kwa muda wa miezi miwili na katika upasuaji huo vimekutwa visu vilivyokunjwa ambavyo vikikunjuliwa vina urefu wa inchi 7 na vingine vimeshika kutu na kukatika.
Mgonjwa huyo alielezea sababu iliyomfanya kula visu hivyo "Sijui kwanini nilikuwa nakula visu, nilikuwa na enjoy tu kama watu wengine wanavyopenda kilevi na vitu vingine vifananvyo"
Madaktari wametoa ripoti kuwa mgonjwa huyo anaendelea vizuri kwa sasa na kukiri kutorudia tabia hiyo ya kula visu na kushukuru madaktari kumuokoa maisha yake ndani ya operesheni ya masaa matano aliofanyiwa.
Social Plugin