NB-Siyo Nyundo iliyotumika katika mauaji Kahama |
Jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga limefanikiwa kumkamata mwanamme anayejulikana kwa jina la Deus Shitungulu anayetuhumiwa kumuua mke wake Monica Dadagada (25) kwa kumpiga nyundo kichwani katika kijiji cha Busungo kata ya Segese halmashauri ya Msalala wilayani Kahama.
Mwanamme huyo anadaiwa kumuua mke wake Agosti 14 mwaka huu majira ya saa nne usiku baada ya kile kilichoelezwa kuwa usiku huo mme wake alipigiwa simu na mwanamke
mwingine ndipo mkewe (Monica) akamuuliza mmewe kuwa mwanamke anayepiga simu
ni nani hali iliyosababisha kuibuka ugomvi na hatimaye jamaa akachukua nyundo na kuitumia kumshambulia mkewe kichwani na kusababisha kifo chake papo
hapo.
Kwa mujibu wa kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Muliro Jumanne Muliro mtuhumiwa huyo amekamatwa na jeshi la polisi baada ya wananchi kushirikiana na jeshi hilo kumsaka katika maeneo mbalimbali kama Busungo,Segese,Lunguya,Kakola,Bulige na hatimaye kumnasa akiwa mjini Kahama.
Kamanda Muliro amesema mtuhumiwa anahojiwa na polisi na atafikishwa mahakamani haraka iwezekanavyo.
SOMA HABARI KAMILI <<HAPA>>
SOMA HABARI KAMILI <<HAPA>>
Social Plugin