Jeshi
la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limesema limejiandaa kudhibiti
maandamano ya Umoja wa Kupambana na Udikteta Tanzania (Ukuta)
yaliyoandaliwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)
yanayotarajiwa kufanyika Septemba Mosi mwaka huu.
Wakati
akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Kamanda wa
Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam Simon Sirro amewatoa
hofu wakazi wa mkoa huo kuwa hakuna mtu na au kikundi chochote cha watu
kitakachofanya maandamano siku hiyo.
“Habari
ya Ukuta haipo,umeshabomoka na kama haujabomoka utabomoka, wakazi wa
Dar es Salaam msiwe na hofu, fanyeni kazi na hata siku hiyo hakuna mtu
atakayejitokeza barabarani kuandamana,” amesema.
Kamanda
Sirro amedai kuwa siasa zinatakiwa kufanywa kwa amani na utulivu na
kwamba wanasiasa wanaoitumia siasa kufanya vurugu hawatafanikiwa.
“Mimi
niwahakikishie kwamba tunajiandaa kwelikweli kuhakikisha watu wanafuata
sheria , anayetaka kuvunja sheria kwa kufanya maandamano aanze yeye ili
nasi tuanze naye,” amesema.
Ameongeza kuwa ”
Suala la utii wa sheria ni la msingi,kama kuna watu au kikundi cha watu
kinataka kuitumia siasa kufanya uvunjifu wa amani wajue kwamba nafasi
hiyo kwa Dar es Salaam haipo.”
Aidha,Kamanda
Sirro amesema August 20 2016 Jeshi la Polisi lilipata taarifa toka kwa
raia wema kuwa maeneo ya Kinondoni kuna duka linauza flana zenye maneno
ya uchochezi yaliyoandikwa ‘’TUJIPANGE TUKATAE UDIKITETA UCHWARA’’ , ‘UKUTA’ ‘
Amesema Polisi baada ya kupata taarifa hizo walifika eneo la tukio na kumkamata mtuhumiwa aitwaye YORAM SETHY MBYELLAH miaka 42, mfanyabiashara na mkazi wa Mburahati akiwa anauza fulana hizo dukani kwake
Amesema Polisi baada ya kupata taarifa hizo walifika eneo la tukio na kumkamata mtuhumiwa aitwaye YORAM SETHY MBYELLAH miaka 42, mfanyabiashara na mkazi wa Mburahati akiwa anauza fulana hizo dukani kwake
Social Plugin