Mkutano
Mkuu Maalum wa Chama Cha Wananchi (CUF), uliofanyika jana jijini Dar es
Salaam ukilenga kuwachagua Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa chama
hicho ulivunjika baada ya wajumbe kuanza kurushiana viti na matusi baada
ya kupishana katika hoja ya kumtosa aliyekuwa Mwenyekiti wake, Profesa
Ibrahim Lipumba.
Profesa
Lipumba alijiuzulu nafasi yake kabla ya kampeni za uchaguzi Mkuu mwaka
jana akieleza kuwa roho inamsuta kumnadi mgombea urais aliyeungwa mkono
na vyama vya Ukawa. Lakini mwaka huu alirejea na kuandika barua akiomba
kurejea kwenye nafasi yake hali iliyozua sintofahamu.
Taarifa
kutoka ndani ya Mkutano huo zimeeleza kuwa wajumbe 832 walihudhuria
lakini hoja ya kumjadili Profesa Lipumba ilipofikiwa, baadhi ya wajumbe
ambao wanamuunga Mwenyekiti huyo wa zamani walizua vurugu wakipinga
utaratibu uliotumika.
Baadhi
ya wajumbe hao waliwaambia waandishi wa habari kuwa viongozi waliopo
madarakani walifanya ubabe kwa kulazimisha kura ya kukubali au kukataa
ombi la Lipumba ipigwe kwa uwazi na sio siri kama Katiba inavyoeleza.
“Haki
haikutendeka, ni ubabe. Wala mkutano haikuzingatia kutimia kwa akidi.
Tulilazimishwa kupiga kura kwa kunyoosha mikono wakati mazingira
yaliyopo na usahihi, kura ni siri,” mmoja wa wajumbe hao alikaririwa.
Baada
ya kupiga kura za wazi, Lipumba alipata kura 14 kati ya kura 832 hivyo
kuonekana kukataliwa kwa kishindo, lakini vurugu zilizuka ghafla
kutokana na maamuzi hayo na mkutano ukashindwa kufanikisha zoezi zima la
kuwapata viongozi hao wapya.
Katika
hatua nyingine, Juma Haji Duni alijiengeu katika kinyang’anyiro cha
uchaguzi huo, baada ya baadhi ya wajumbe kusisitiza kuwa katiba inamtaka
mtu aliyejiuzulu na kuhamia chama kingine kusubiri miaka miwili ili
agombee nafasi ya uongozi ndani ya chama pale atakaporejea.
Mkurugenzi
wa Uchaguzi na Mipango wa CUF, Shaweji Mketo, alisema kuwa Duni
alijiondoa kutokana na maadui wa Ukawa kutaka kukihujumu chama hicho.
Mkutano huo umeahirishwa hadi utakapotangazwa tena.
Social Plugin