Mahabusu
aliyekuwa akishikiliwa katika kituo kikuu cha polisi jijini Arusha
aliyetambulika kwa jina la Victoria Wenga (51) mkazi wa Lemara jijini
Arusha amejinyonga hadi kufa usiku wa kuamkia jana kwa kutumia shuka
lake bila kuacha ujumbe wowote.
Marehemu
alikamatwa Agosti 21 mwaka huu majira ya Alfajiri kwa tuhuma za kuchoma
moto nyumba yake na maduka yake mawili kutokana na ugomvi wa kifamilia.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo alikiri kutokea kwa tukio hilo
katika Kituo cha Kikuu cha Polisi saa 6:20 usiku jana wakati wenzake
wakiwa wamelala.
“Polisi
wa zamu alisikia kelele kutoka kwenye chumba cha mahabusu wa kike
ambapo polisi walijitahidi kuokoa maisha ya mahabusu huyo, lakini
ilishindikanika,” alisema Kamanda Mkumbo.
Mahabusu
huyo, ambaye ni mkazi wa Lemara jijini Arusha, alijinyonga kwa kutumia
shuka lake alilokuwa anatumia kujifunikia wakati yuko mahabusi.
Mtuhumiwa huyo, alijinyonga kabla ya kufikishwa mahakamani kujibu
mashitaka yake.
“Jana ilikuwa afikishwe mahakamani kujibu kosa lililokuwa linamkabili,” alisema
Kamanda Mkumbo na kuwahakikishia kuwa hali ya usalama kituoni hapo na
tukio hilo, havihusiani na sababu zozote za kiusalama.
Marehemu
Victoria anadaiwa kuwa na ugomvi wa kifamilia na mume wake
aliyetambulika kwa jina la Edward Wenga akimtuhumu kuzaa nje ya ndoa
kinyume na utaratibu.
Imeelezwa
kuwa hicho ndo chanzo cha marehemu kufikia hatua ya kuteketeza mali
walizochuma na mume wake ambazo ni maduka mawili na nyumba ya kuishi.
Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika chumba cha kuifadhia mahiti Hospitali ya Mount Meru.
Social Plugin