Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

Makubwa Haya!! Marehemu Aongezwa Kwenye Picha za Harusi


Bi harusi, ambaye kakake alifariki wiki chache kabla yake kufunga ndoa, amechukua hatua isiyo ya kawaida kwa kuongeza picha za kakaake huyo katika zake za harusi Uingereza.


Kakaake Catherine Carter, Shaun Carter, alifariki kwenye ajali Mei lakini alipofunga pingu za maisha Julai aliomba usaidizi kutoka kwa mtaalamu wa picha kuongeza picha za Shaun kwenye picha za harusi.

Katika picha moja, Catherine anaonekana akiwa na mamaake na babake wa kambo na kwenye picha ambayo haijakolea sana na nduguye anayeonekana kuweka mikono yake kwenye bega la Catherine.

Alisema: "Ni mwujiza kumuona kwenye picha zangu za harusi, sikuweza kujizuia kutokwa na machozi."

Seeing him in the pictures was a miracle, I couldn't stop crying."
 

'Heartbreaking'

Shaun, 29, alifariki katika ajali eneo la mjengo Cirencester, eneo la Gloucestershire, mwishoni mwa mwezi Mei.

Catherine, aliolewa na John Flower katika kanisa la St Paul's, Chippenham mwezi Julai.


 Catherine anaonekana akiwa na mamake na babake wa kambo na kwenye picha ambayo haijakolea sana na nduguye anayeoneakana kuweka mikono yake kwenye bega la Catherine.

Rachel, wa kampuni ya Jelly Penguin Graphics, ambayo iliunda picha hizo, amesema ombi la Catherine lilimgusa sana.

Tangu picha hizo zipakiwe kwenye Facebook, zimependwa na zaidi ya watu 2,000 na mamia ya watu wametolea maoni.
Via>>BBC
mwezi Julai.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com