Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

Mashabiki wa Yanga Waibuka Ofisi za Makao ya Klabu Hiyo Baada ya Yusuph Manji Kujiuzulu Kwa Sababu 2 za Msingi

Yusuph Manji

Yusuph Manji

Mashabiki wa Yanga wakiw katika ofisi za makao makuu ya klabu ya Yanga baada ya kupata taarifa za kujiuzulu kwa Manji

*****
Habari zilizoenea kwenye mitandao ya kijamii ni kwamba Mwenyekiti wa Yanga Yusuf Manji ameamua kujiuzulu wadhifa wa uenyekiti katika klabu hiyo pamoja na kusitisha zoezi la kutaka kuikodi timu hiyo kwa miaka 10 kama ilivyokuwa dhamira yake hapo awali.



Sababu mbili zinazodaiwa kumfanya Yusuph Manji amejiondoa ndani ya Yanga ni kusemwa na baadhi ya viongozi wa serikali na baadhi ya viongozi wa Yanga ambao wanatajwa kutumiwa na baadhi ya wafanyabiashara kwa maslahi yao binafsi, bado Manji hajatangaza rasmi kupitia vyombo vya habari.



Kwa mujibu wa vyanzo vya ndani ya Yanga, inadaiwa kuwa bosi huyo ameamua kukaa pembeni ikiwa ni baada ya kuibu kwa mijadala mikubwa na baadhi ya watu kupinga uamuzi wake wa kutaka kuikodi Yanga.



“Natukanwa sana na baadhi ya matajiri ambao ni wapenzi wa Yanga…hawapendi mimi niwepo pale. Pesa ni yangu natoa kwa mapenzi niliyonayo kwa klabu yangu…kwanini nitukanwe wakati sipati maslahi yoyote? Najiuzulu,” Ni kauli ya mwenyekiti wa Yanga SC ambaye ametangaza kujiuzulu kufuatia kusakamwa na hasa baada ya kuomba kuichukua Yanga kwa miaka 10. (kwa mujibu wa facebook page ya Naipenda Yanga).



Hata hivyo kumekuwa na vikao mbalimbali kumsihi Manji abadili maamuzi yake lakini inaonekana amechoka na ameamua kuibwaga Yanga.



Tayari Reginald Mengi ameonesha nia ya kuingia Yanga endapo Manji ataondoka. Leo jioni baraza la wazee linataraji kuwa na kikao na Mengi.



Baada ya Mwenyekiti wa Yanga Yusuf Manji kutangaza kujiuzulu nafasi hiyo, Mashabiki na wanachama wa Yanga wamekusanyika kwenye ofisi za klabu hiyo wakipinga kujiuzulu wakipinga kujiuzulu kwa mwenyekiti wao.



Baadhi ya wanachama na mashabiki wamekuwa wakidai kwamba kuna watu ambao hawataki kumuunga mkono Manji katika zoezi zima la kutaka kuikodi timu pamoja na nembo kwa miaka 10.



Mzee Akilimali amekuwa akitajwa kuwa miongoni mwa watu wanaopinga kusudi la mwenyekiti wa klabu hiyo Yusuf Manji kuikodi klabu hiyo.

 Taarifa nyingine kutoka Ukurasa wa Facebook wa Naipenda Yanga Yangu unasomeka ifuatavyo:

"TAAARIFA SAHIHI IKIWA IMETOKA KWA KATIBU KUHUSIANA NA MWENYEKITI KUJIWEKA PEMBENI. 

Ni kweli Mwenyekiti amekusudia kufanya hivyo kwa sababu anasakamwa , anatukanwa na kudhalilishwa na Makonda na Mzee Akilimali.

Lakini kibaya hakuna tamko kutoka kwa Mwana-Yanga yeyote aliyekemea hilo na kuonyesha kumuunga mkono MWENYEKITI .Hivyo anajiona mnyonge na amesuswa bora akae pembeni. . Hivyo tumewasiliana viongozi wa Kanda wote tumeamua Tuitishe kikao cha Dharula kesho SAA 4 Asubuhi pale makao makuu tutatoa Tamko la pamoja na wengine wataanza kuongea na vyombo vya habari Leo hii.
Hima Tuhamasishane tuwe pamoja kesho .Tuwasihi wanachama wetu wafike club.
Katibu Mkuu."

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com