Mhubiri mmoja wa kikristo huko nchini Nigeria ,Pastor Enoch Adejare Adeboye amezua gumzo kali baada kutoa wito kwamba wavulana na makapela wengine wasioe wasichana wasiojua kupika.
Pastor Enoch Adejare Adeboye ambae ni msimamizi wa kanisa liitwalo Redeemed Christian Church of God,alitoa wito huo wakati wa hotuba zake kanisani humo, ambazo pia hutangazwa kwenye televisheni.
"usioe msichana ambae hajui kupika!" Pastor Enoch Adejare Adeboye amewasisitizia mabwana harusi watarajiwa huku akiongeza ' "usioe msichana eti kwa sababu tu anaweza kuimba!Oa msichana anaemuabudu Mwenyezi Mungu, anaeweka kutekeleza maombi kwa Mwenyezi Mungu kisawasawa! Kama hawezi kufanya maombi kwa mda wa saa moja, usimue , usioe msichana mvivu ! Usione asiyejua kupika, kwani utakuwa kila siku unakula mahotelini? Huwezi kumudu hizo gharama za kula kwenye migahawa kila mara ?
Ujumbe huo ambao umerekodiwa kwenye ukanda wa video sasa uko juu kwenye chati za mitandao ya kijamii baada ya kusambazwa na wengi walioskia.
Baadhi wametoa maoni yao kupitia facebook na twitter, na ni bayana kuwa wanaoufanyia mzaha ujumbe huo, huku wengine wakiona kama uchochezi dhidi ya wanawake au kuingilia maswala ya ndoa za watu lakini pia wapo ambao wanamuunga mkono kwa dhati mhubiri wao.
Via>>BBC Swahili
Social Plugin