Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Muliro Jumanne Muliro. |
Mwanamke aliyejulikana kwa jina la Monica Manyabhuluba mkazi wa kijiji cha Busungo kata ya Segese wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga ameuawa kwa kupigwa nyundo kichwani na mme wake Deus Shitungulu
Akizungumza na Malunde1 blog, diwani wa Kata ya Segese Joseph Manyala amesema tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo.
“Chanzo ni wivu wa mapenzi kwani mwanamme alipigiwa simu usiku na mwanamke mwingine,mkewe (Monica) akamuuliza mmewe huyo mwanamke anayekupigia simu usiku huu ni nani ndipo ugomvi ukaibuka na hatimaye jamaa akamuua mke wake kwa kumpiga nyundo kadhaa kichwani na kusababisha kifo chake papo hapo”,amesema diwani huyo.
“Kichwa cha mwanamke huyo kimebondeka kwa kupigwa nyundo,kwa kweli tukio hili linasikitisha sana,polisi wamefika eneo la tukio mchana huu”,amesema Manyala.
Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Muliro Jumanne Muliro amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuongeza kuwa mtuhumiwa amekimbia na juhudi za kumtafuta zinaendelea.

Social Plugin