Mkuu
wa Mkoa wa Mwanza, Mhe.John Mongella (kulia) akitoa taarifa ya ujio wa
Rais Magufuli mkoani Mwanza. Kushoto ni Katibu Tawala mkoani Mwanza,
CP.Clodwig Mtweve.
****
Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli, anatarajia kufanya ziara fupi ya kikazi mkoani Mwanza.
Mkuu
wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella, leo amesema, Rais Magufuli atafanya
ziara ya siku mbili kuanzia kesho agost 10 na 11, ambapo atapokelewa
hiyo kesho wilayani Sengerema akitokea Chato mkoani Geita alikokuwa na
mapumziko mafupi.
"Rais
Magufuli atawasili kesho asubuhi katika mkoa wetu akitokea Chato mkoani
Geita na ataanza ziara katika wilaya ya sengerema kwa ajili ya
kuwasalimia wananchi, kuwapa taarifa za mikakati na maendeleo awamu ya
tano pamoja na utekelezaji wa ilani ya uchaguzi". Amesema Mongella.
Pia
amesema hiyo kesho Rais Magufuli atasimama maeneo mbalimbali kwa ajili
ya kuwasalimu wananchi kabla ya kuwasili wilayani Nyamagana.
Ametanabaisha
kwamba Rais Magufuli ataitimisha ziara yake kesho kutwa agost 11, kwa
kukagua ujenzi wa daraja la watembea kwa miguu la Furahisha Jijini
Mwanza, pamoja na upanuzi wa barabara ya Furahisha hadi Pasiansi ambapo
ataweka jiwe la msingi katika ujenzi wa miundombinu hiyo.
Mongella
amewasihi wananchi kujitokeza kwa wingi katika mkutano wa hadhara
utakaofanyika kuanzia majira ya saa nanne mchana katika uwanja wa
Furahisha ambapo Rais Magufuli atahutubia wananchi baada ya kukagua
miradi hiyo ya ujenzi.
Na Judith Ferdinand (BMG), Mwanza
Social Plugin