Najua
litazua maswali, lakini Kwa kuwa litaokoa maisha ya wanawake wajawazito
wa nchi yetu (CEmOC) na wananchi wengine, nimelitoa. Nitalitetea.
Nitalisimamia!
Nimeagiza
maDED na maDMO wote nchini kuhakikisha wana theatres ZENYE KUFANYA KAZI
IPASAVYO kwenye vituo vyote vya Afya kwenye maeneo yao. Wiki iliyopita
nilitembelea Manispaa ya Ilala, kwenye vituo vya afya vitatu
nilivyotembelea hakukuwa na theatre yenye kufanya kazi.
Kwa
mujibu wa sera ya afya ya Tanzania, 'kituo cha afya' kitakuwa na hadhi
hiyo kama kina uwezo wa kufanya upasuaji. Vinginevyo hiyo ni zahanati.
Mara nyingi watendaji hawa wamekuwa wakijificha kwenye kichaka cha
'hatuna fedha', wengine wakiomba fedha kutoka serikali kuu.
Nilimuuliza
Mkurugenzi wa Ilala, unakusanya sh ngapi Kwa mwezi, akasema bilioni 6.
Nikamuuliza unadhani ni sh ngapi kuwa na theatre yenye kufanya kazi?
Akakosa jibu. Nikampa miezi 6 awe na theatre zenye kufanya upasuaji.
Leo(jana)
nimefanya ziara yangu mikoa ya Shinyanga na Simiyu, nikitimiza mikoa
24. Huku pia nimekutana na tatizo hilo hilo nilipokuwa Kishapu,
Shinyanga na Mwanhuzi, Simiyu. Hawa wa Meatu wenyewe wana kituo cha Afya
Mwandoya, takriban Km 60 kutoka Hospitali ya Wilaya ya Meatu, pale
Mwanhuzi. Wamekipa uwezo wa kufanya upasuaji. Wamenunua vifaa, wameajiri
hadi Daktari (MD) kwa ajira ya muda kwa ajili ya kufanya kazi pale.
Kituo
kimefanya takriban operation 40, zote salama Kwa asilimia 100.
Wamepunguza msongamano Mwanhuzi na wamepeleka huduma nyeti na za kuokoa
maisha Karibu zaidi na wananchi, ukizingatia huku hakuna barabara za
lami na hakuna ambulances. I was impressed.
Nikasema
sababu za kuwa Halmashauri hazina pesa huku zinakusanya mamilioni
ambayo wanayatumia bila ku-address matatizo ya msingi ya wananchi
hazikubaliki. Leo iwe mwisho. Nimeagiza wakurugenzi wa Halmashauri zote
nchini washirikiane na maDMO wajue watakavyofanya wahakikishe wanafungua
huduma za upasuaji kwenye vituo vyote vya afya nchini ndani ya miezi
sita (6).
Baada
ya miezi hiyo sita mimi mwenyewe na timu yangu ya kurugenzi ya ukaguzi
na uhakiki ubora wa huduma za afya (inspectorate and quality assurance)
tutasambaa nchi nzima kukagua huduma hizi na pale ambapo hatutozikuta
tutakishusha hadhi kituo hicho kutoka ngazi ya 'kituo cha afya' na kuwa
ngazi ya 'zahanati' sambamba na kuwashauri wenzetu wa Ofisi ya Rais,
TAMISEMI kuwa wakuu hao wa idara wameshindwa kutekeleza majukumu yao na
hivyo wawashushe vyeo.
Nitasimamia uamuzi huu Kwa nguvu zangu zote. Sababu ni kwamba ninajua faida yake. Ninajua Mungu atafurahi, atanibariki.
Wakati
wa Bunge la bajeti wanaharakati wa haki za wanawake na Watoto
waliwahamasisha Wabunge watushughulikie Kwa ajili ya suala hili.
Wakawa-pump wabunge data kuwa kwa siku magnitude ya vifo vinavyotokana
na sababu za uzazi ni sawa na 'coaster' moja ipate ajali na iue watu
wote! Wabunge waligeuka mbogo. Japokuwa namba hizi zilikuwa exaggerated
(zilizidishwa), walifikisha point kwetu. Kwamba lazima tufanye kitu
tofauti kwenye eneo hili. Mimi naanza kuchukua hatua. Vifo vitokanavyo
na uzazi havikubaliki!
Dkt. Hamisi Kigwangalla, MB., NW-AMJW.
August 18th, 2016.