Mchungaji mmoja nchini Afrika ya kusini kwa jina la Lethebo Rabalango wa kanisa la Mount Zion General Assembly amemua muumini wake ambaye ni mwanamke kwa kumwekea spika nzito juu yake kwa muda wa dakika tano kupima nguvu ya uwepo wa mungu na kwamba hatahisi maumivu yoyote.
Mchungaji Lethebo alimwalika mwanamama huyo mbele ya kanisa ili aweze kuonesha miujiza ya Mwenyezi Mungu, ndipo alipomwamuru mwanamke huyo alale chini na kuwaambia watumishi wa kanisa wamwekee spika juu yake yenye uzito wa 113.4k na mchungaji kukaa juu yake kwa nia ya kumkandamiza.
Mchungaji huyo alisema kwa uwezo wa Mungu mwanamke huyo hatahisi maumivu, ila cha kushangaza mwanamke alibakia kimya baada ya kukosa pumzi,na kusemekana kuwa amepoteza fahamu.
Juhudi za kumwamsha ziligonga mwamba ndipo ikabainika kuwa mwanamama huyo amepoteza uhai.

Hata hivyo mchungaji amemlaumu marehemu kwa kusema kwamba hakuwa na imani ya kutosha.
Social Plugin