China ni miongoni mwa Mataifa makubwa duniani ambapo uchumi wake unazidi kukua pamoja na miundombinu yake, ndiyo nchi pekee inayoongoza kwa miundombinu ya madaraja yaliyovunja rekodi kwa ubora duniani, hivi karibuni imeripotiwa kuzunduliwa kwa daraja lililotengenezwa kwa vioo.
Daraja la kioo ambalo limeelezwa kuwa liko juu zaidi limezinduliwa hivi karibuni nchini China ambapo lina urefu wa zaidi ya futi 1400, upana wa futi 20 na karibu futi 1000 kutoka kwenye ardhi na imeripotiwa kuwa kioo chake ni imara zaidi mara 25 zaidi ya kioo cha dirisha.
Daraja hilo la wapita kwa miguu lijulikanalo kwa jina la daraja la Zhangjiajie limezinduliwa July mwaka huu ambapo lina uwezo wa kuchukua watu hadi 800 kwa wakati mmoja. Imeelezwa kuwa daraja hilo limekuwa likitumika kwa shughuli mbalimbali za kiutalii.
.
.
Sehemu hii ni ya nyongeza ya daraja hilo la vioo